Balozi Mindi Kasiga ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya serikali kwa Umma akizungumza na wanahabari kwenye Wiki ya Ubunifu Tanzania iliyondaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kupitia Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) linaloendelea jijini Dar es Salaam ambapo kilele chake kinatakuwa Mei 16, 2022 jijini Dodoma.
Msaidizi wa Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania Job Runhaar akizungumza kuhusu hatua ambazo wanachukua nchi yao inachukua katika kusaidia sekta ya ubunifu nchini.
Mkurugenzi wa Kodi kutoka Kampuni ya KPMG Bw. Donald Nsanyiwa akizungumza na wanahabari mara baada ya kutoa mada iliyokuwa ikielezea umuhimu wa wabunifu wakuwemo wajasiriamali na wafanyabiashara kuwa na utamaduni wa kutambua masuala yanayohusu ulipaji kodi.
Mmoja ya Vijana wakitanzania ambaye ameshiriki kwenye Wiki ya Ubunifu Tanzania inayoendelea Ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam akielezea shughuli ambazo amekuwa akizifanya kupitia kampuni anayofanyia shughuli zake zinazotuokana na masuala ya kibunifu.
Mmoja ya washiriki akifafanua jambo wakati wa kongamano la wabunifu ambalo lilikuwa likijadili masuala yanayohusu umuhimu wa wabunifu kutambua masuala yanayohusu kodi.

Na Cathbert Kajuna - Kajunason, Dar es Salaam.

Wizara ya Mambo ya Nje na Uhusiano wa Afrika Mashariki imewahakikishia ushirikiano wabunifu wa Tanzania katika kuwatangaza kimataifa ili waweze kufikia malengo yao.

Kauli hiyo imetewa na Balozi Mindi Kasiga ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya serikali kwa Umma alipokuwa akizungumza kwenye Wiki ya Ubunifu Tanzania iliyondaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kupitia Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) linaloendelea jijini Dar es Salaam ambapo kilele chake kinatakuwa Mei 16, 2022 jijini Dodoma.

Wizara hiyo imesema inataka kuona kunakuwa na wabunifu wengi zaidi ambao wanaibuliwa nchini kila siku na kwamba wabunifu wasikubali kuwa kimya badala yake wajitokeze na kwenda kutambuliwa na mamlaka husika.

“Niko hapa leo kwa ajili ya shughuli hii ya Wiki ya Ubunifu Tanzania inayoratibiwa na Ubalozi wa Uholanzi nchini Tanzania. Cha muhimu ambacho tumejifunza kutokana na mazungumzo tuliyoyafanya na wabunifu wa kitanzania kuna mambo ambayo yamejitokeza katika mazingira ya sasa hususani kwenye utali ambao ni muhimu sana kuhusisha ubunifu.

“Hatuwezi kuendelea kutangaza utalii kwa njia zile zile za zamani ndio maana mpaka sasa hivi tunaona Rais wa Samia Saluhu Hassan akiendelea kufanya promosheni ya filamu ya Royal Tour inayoelezea vivutio vya utalii Tanzania kama nchi ya kipekee katika eneo la utalii,”amesema Balozi Kasiga.

Amesema kuwa Wiki ya Ubunifu Tanzania kupitia majadiliano yaliyofanyika leo wamejadili kwa kina nini kifanyike kwenye ubunifu kwa njia mbadala ya kutangaza na kuvutia watanzania kwenda kwenye utalii wa Tanzania.

“Kwa hiyo tulikuwa na mjadala tunaposema kutangaza utalii tunaanza na sisi wenyewe?Tunaanzaje au wanaanza Wazungu? tukaona yote yanahitajika na yote ni muhimu,” amesema Balozi Kasiga alipoelezea ubunifu katika kutangaza utalii.

Amefafanua kuwa majadiliano hayo wameangalia ni jinsi gani wanaweza kutumia teknolojia na ubunifu kama njia mojawapo ya kuleta maendeleo huku akitumia nafasi hiyo kumuelezea Mtanzania Idd John ambaye amekuja na ubunifu wa jukwaa la Safari Wallet.com.

“Jukwaa hilo unaweza kuingiza fedha kutoka kwenye simu yako ya kiganjani na ukaenda kutalii sehemu yoyote Tanzania. Kwa kutumia Wallet Safari kwanza unaweza kulipa fedha na kwenda kutalii kokote hapa nchini.

“Hivyo ni wajibu wetu Wizaara ya Mambo ya Nje pamoja na Watanzania wengine kuangalia tunafanya nini kumsaidia Idd aliyebuni Wallet Safari, sisi kwa nafasi yetu tunasema tutampka kila aina ya ushirikiano na ndio wajibu wetu kumsadia kila Mtanzania ,kwa kutumia balozi zetu tutamsaidia kutangaza jukwaa hilo,” amesema.

Balozi Kasiga ameeleza Wizara yao ni kiungo kiunganishi nchi za nje ambapo kuna wawakilishi (mabalozi) na wakati huo huo mataifa mengine nayo yanawawakilishi wao hapa nchini.

Kwa upande mwingine, mtoa mada katika majadiliano yaliyohusisha wabunifu na masuala ya kikodi Bw. Donald Nsanyiwa ambaye ni Mkurugenzi wa Kodi wa Kampuni ya KPMG amesema moja ya jambo la msingi linalopaswa kuzingatiwa ni kufahamu masuala ya kodi.

“Tumejaribu kuwalezea wabunifu wakiwemo wanaojihusisha na ujasiriamali kuwa wanapoona watu wa TRA wanakuja kwenye biashara zao wasione kama wanawaingilia bali jukumu lao kubwa ni kuwapa elimu ya kujua umuhimu wa kodi pindi wanapoanza biashara,” amesema.

Wiki ya Ubunifu Tanzania ambayo kilele chake kitafanyika Dodoma Mei 16, 2022 inaratibiwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ikishirikiana na COSTECH na UNDP kupitia programu ya Ubunifu - FUNGUO huku mdhamini mkuu akiwa Vodacom Tanzania.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: