Makamu wa pili wa rais wa Zanzibar mhe. hemed Suleiman Abdulla akifanya mazungumzo na Muwakilishi wa Shirika la Chakula Duniani Nchini Tanzania Bi Sara Gordon-Gibson alipofika Ofisi kwake Vuga Jijini Zanzibar alipofika kubadilishana nae mawazo pamoja na kumkabidhi mpango kazi wa miaka mitano 2022-2027
---
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amepongeza juhudi zinazofanywa na Shirika la Chakula Duniani kwa kusaidia maendeleo Nchini.

Mhe. Hemed ametoa Pongezi hizo alipokutana na kufanya mazungumzo na Muwakilishi wa Shirika hilo Nchini Tanzania Bi Sarah Gordon-Gibson na ujumbe wake walipofika Ofisini kwake Vuga Jijini.

Amesema Serikali inathamini Mchango unaotolewa na Shirika hilo na kupongeza Mkakati wao wa kuandaa mpango kazi wa miaka mitano ijayo ambao umelenga zaidi kuangalia maeneo mbali mbali ikiwemo Kusaidia kina mama katika uvuvi na ukulima wa mwani pamoja na mazao yote yanayotokana na bahari.

Aidha Mhe. Hemed ameeleza kuwa katika mazungumzo hayo shirika la Chakula Duniani limepanga kuangaza katika eneo la kukabiliana na Maafa ambapo tayari wataalamu wameanza kukaa pamoja kuangalia namna bora watakayotumia katika eneo hilo ili kufikia malengo waliojipangia.

Sambamba na hayo Mhe. Hemed ameeleza kuwa mategemeo ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuwa Mpango kazi wa Miaka mitano ijayo wa Shirika hilo ni kuwa na utendaji bora zaidi kwa kuangalia maslahi ya wananchi.

Pamoja na mambo mengine Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ameeleza kuwa Dunia imeathirika na athari zinazotokana na Vita kati ya Ukraine na Urusi ambapo Zanzibar inapokea ushauri na juhudi zaidi zinahitajika ili kuwahurumia wananchi wake.

Aidha Mhe. Hemed ameeleza kuwa Serikali kwa kushirikiana na mashirika mbali mbali iko tayari kuangalia namna ya kunusuru Uchumi ili kumsaidia Mwananchi asiathrike na majanga hayo.

Kwa upande wake Muwakilishi wa Shirika la Chakula Dunia Nchini Tanzania Bi Sarah Gordon-Gibson amemueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kuwa Mpango kazi wa miaka mitano ijayo utakaoanza Mwezi Julai 2022 wamejipanga kusaidia kina mama kwa kuwapa mafunzo, vitendea kazi pamoja na kuwasiadia kutafuta soko la bidhaa zao ili kupata ufanisi wa kazi.

Aidha Bibi Sarah ameeleza kuwa Mpango kazi huo utaangalia zaidi hali ya kimaumblie ili kuweza kuwasaidia Wananchi wa Tanzania katika maeneo yenye uhitaji zaidi.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: