Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinwumi Adesina leo tarehe 10.02.2022 amefanya ziara ya siku moja Wilayani Chato yenye lengo la kutoa salamu za pole kwa familia ya hayati Dkt. John Pombe Magufuli.

Dkt. Adesina amepokewa katika uwanja wa ndege wa Geita uliopo Chato na kaimu Mkuu wa Wilaya ya Chato ndugu Wilson Shimo pamoja na kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya.

Akiwa nyumbani kwa hayati Dkt. John Pombe Magufuli Dkt. Akinwumi Adesina amesema amefika nyumbani kwa hayati Magufuli kutokana na urafiki mkubwa aliokuwa nao na hayati Rais Maguli pamoja na kutambua mchango mkubwa ambao hayati Magufuli aliutoa kwa watanzania na kwa watu wengine. “Rais Magufuli alikuwa mfano mzuri kwa viongozi barani Afrika, aliwapenda watanzania na waafrika wote kwa moyo wake wote” alisema Dkt. Adesina.

Rais wa AfDB amesema pamoja na kuodokewa na Rais Magufuli anafarijika kuona Tanzania bado ipo kwenye mikono salama chini ya Rais Samia Suluhu Hassan ambaye anaendeleza yale yote mazuri yaliyoachwa na hayati Magufuli.

Dkt. Akinwumi Adesina amemshukuru Rais Samia kwa ushirikiano na kumruhusu kufika Wilayani Chato kwa ajili ya kutoa salamu za pole. Dkt. Akinwumi Adesina na ujumbe ulioambatana naye wamerejea jijini Dar es Salaam.
Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinwumi Adesina katika matukio ya uwekaji wa shada kwenye kaburi la hayati Dkt. John Pombe Magufuli
Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinwumi Adesina akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato ndugu Mandia Kihiyo.
Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinwumi Adesina akisalimiana na Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Chato Ndugu Wilson Shimo wakati Rais huyo alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Geita uliopo Chato leo Tarehe 10. 02.2022
Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinwumi Adesina akisalimiana na Katibu Tawala Mkoa wa Gita Ndugu Musa Chogero wakati Rais huyo wa AfDB alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Geita uliopo Chato leo Tarehe 10. 02.2022
Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinwumi Adesina akisalimiana na mdogo wa hayati Dkt. John Pombe Magufuli ndugu Gorodian Joseph Magufuli nyumbani kwa hayati Magufuli Mlimani kata ya Muungano Wilayani Chato.
Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinwumi Adesina akiwa kwenye picha ya pamoja na maafisa wengine walioambatana na Rais huyo wa AfDB na Mdogo wa hayati Dkt. John Pombe Magufuli ndugu Gorodian Joseph Magufuli nyumbani kwa hayati Magufuli Mlimani kata ya Muungano Wilayani Chato.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: