Mhandisi Mwandamizi wa Tanroad mkoa wa Ruvuma Justine Mrope wa kwanza kushoto, na meneja wa kiwanja cha ndege cha Songea Jordan Mchami wa pili kushoto wakiwa na wawakilishi wa Kampuni ya Chico inayofanya kazi ya upanuzi wa kiwanja cha ndege cha Songea wakikagua kazi mbalimbali katika kiwanja hicho.
Waandisi wa Tanroad mkoa wa Ruvuma na wakandarasi wa mradi wa kiwanja cha ndege cha Songea wakijali kuhusu kukamilika kwa ujenzi wa kiwanja cha ndege cha Songea mkoani Ruvuma ambapo kimekalimika kwa asilimia 90.
Sehemu ya kuruka na kutua ndege katika kiwanja cha ndege cha Songea mkoani Ruvuma.

Na Muhidin Amri, Songea

SERIKALI kupitia wakala wa Barabara nchini(Tanroad)mkoa wa Ruvuma, imetumia Sh.bilioni 37,090,185,911.00 kufanya upanuzi wa kiwanja cha ndege cha Songea mkoani humo, kilichoanza kujengwa Mwezi April 2019.

Hayo yamesemwa na Kaimu Meneja wa Tanroad mkoa wa Ruvuma Mhandisi Ephatar Mlavi,wakati akizungumzia ujenzi wa uwanja huo ambapo alisema hadi sasa ujenzi wake umekamilika kwa asilimia tisini.

Alisema,kazi zilizofanywa na Mkandarasi kampuni ya Chico katika mradi huo ni kujenga barabara ya kutua na kuruka ndege,kujenga ofisi ya Mhandisi mshauri ambayo baada ya kazi kuisha itakuwa jengo la muda la abiria,kujenga maegesho na jengo la kuweka jenereta(Power House) ambapo ujenzi wa njia za kuruka na kutua ndege zimekamilika na uwanja umeanza kutumika.

Alisema,tayari Mkandarasi ameshalipwa jumla ya Sh.19,555,560,906.98 na mradi ulikamilika tangu Mei 2021 na sasa upo kwenye muda wa matazamio ambapo Mkandarasi anaendelea na kazi ndogo ndogo.

Mhandisi Mlavi alitaja kazi zilizobaki ambazo zinazoendelea, ni kujenga jengo la kuongozea ndege(Control Tower)ufungaji wa taa,ufungaji wa mifumo ya umeme,mifumo ya mawasiliano na ununuzi wa gari la zimamoto.

Kwa upande wake Meneja wa kiwanja cha ndege cha Songea Jordan Mchami alisema baada ya matengenezo hayo uwanja huo kwa sasa una uwezo wa kutua ndege mbalimbali ikiwamo Bombadier.

Alisema, tangu kupunuliwa kwa uwanja huo kumefungua fursa ya kiuchumi kwa wakazi wa mkoa wa Ruvuma ambapo idadi ya abiria wanatumia usafiri wa ndege imeongezeka na kupungua kwa nauli.

Mchami, ameiomba Serikali kujenga jengo la abiria kwani lililopo ni dogo linalotosheleza kukaa abiria 50 ikilinganisha na idadi ya watu wanaofika katika kiwanja hicho kwa ajili ya kusafiri.

Aidha,amewahimiza wakazi wa mkoa huo na mikoa jirani kuendelea kutumia usafiri wa ndege ambao ni rahisi kuliko usafiri wa basi katika kufanya shughuli mbalimbali za kiuchumi na kuyaomba mashirika mengine kuleta ndege zao mkoani Ruvuma kufuatia kukamilika kwa upanuzi wa uwanja huo.

Mmoja wa wakazi wa mtaa wa Ruhuwiko Manispaa ya Songea Jeremiha Malon ameishukuru Serikali ya awamu ya sita kuleta mradi wa upanuzi wa kiwanja cha ndege kwani umesaidia sana kuleta ajira.

Pia alisema,kuletwa kwa mradi huo kumepunguza vitendo vya uharifu hasa kwa vijana wa Songea na kuongeza idadi ya watalii wanaofika kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Nyerere.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: