Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Wawakilishi Mheshimiwa Dr Hussein Ali Mwinyi akimkabidhi tuzo ya kutambuliwa kuwa Mlipakodi mkubwa kwa mwaka 2020/2021 kwa Mkurugenzi wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna wakati wa Kongamano la uwekezaji lililofanyika mjini Unguja visiwani Zanzibar leo 7/12/2021.

Na Mwandishi wetu, Zanzibar

SERIKALI imewatambua na kuwapa tuzo walipakodi wakubwa ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru wa Tanganyika.

Tuzo hizo zimetolewa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dr Hussein Ali Mwinyi wakati wa Kongamano la uwekezaji lililofanyika mjini Unguja visiwani Zanzibar

Katika tuzo hizo kampuni ya bia Tanzania Breweries Limited imeibuka ya kwanza ikifuatiwa na kampuni ya uchimbaji wa Dhahabu Geita Gold Mining na nafasi ya tatu imeshikwa na Benki ya NMB.

Takwimu zinaonesha kuwa kampuni ya TBL imechangia kiasi cha Shilingi bilioni 422 wakati kampuni uchimbaji wa Dhahabu ya Geita Gold Mining imechangia kiasi cha Shilingi bilioni 338 na benki NMB ikiwa imechangia kiasi cha Shilingi bilioni 252.

Kwa upande wa Zanzibar kampuni ya usafirishaji ya Azam marine imeibuka ya kwanza kwa kulipa kodi ya Shilingi milioni 930 na nafasi ya pili imeshikwa na Z hotel limited imelipa kodi ya jumla Shilingi milioni 436.

Naye Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Alphayo Kidata amewapongeza walipakodi waliopata tuzo na kutambuliwa na kuwa TRA inathamini sana mchango wa makampuni na taasisi zote zinazolipakodi na tuzo hizi ni kuchochea ulipaji kodi kwa hiari.

Kwa upande wake Kamishna wa walipakodi wakubwa kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) amesema serikali kupitia TRA imewatambua walipakodi hawa wakubwa ili kutoa hamasa kwa walipakodi wengine waweze kulipa kodi kwa hiari na kwa wakati ili serikali iweze kuwahudumia watanzania wote kwa kuwapatia huduma bora.

"Huu ni utamaduni ambao tumekuwa nao kwa miaka mingi sasa, lengo likiwa ni kuongeza mapato yatokana na ulipaji kodi kwa hiari na kwa wakati, nawahamasishe walipakodi wote kulipakodi ili watambulike na waone fahari ya kuwa Mlipakodi mkubwa" amesema Kamishna Mregi.
Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Wawakilishi Mheshimiwa Dr Hussein Ali Mwinyi akimkabidhi tuzo ya kutambuliwa kuwa Mlipakodi mkubwa kwa mwaka 2020/2021 kwa mwakilishi wa Geita Gold Mining wakati wa Kongamano la uwekezaji lililofanyika mjini Unguja visiwani Zanzibar leo 7/12/2021.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: