Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Ng'wilabuzu Ndwata Ludigija (katikati) akiongoza Mbio za kujifurahisha (FunRun) zilizoandaliwa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) na kufanyika jijini Dar es Saaam zilizokuwa na umbali wa Kilometa 5 na 10. Wa pili kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Hamza Johari.
Katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya Usafiri wa Anga Duniani, Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imeandaa Mbio za kujifurahisha(FunRun) kwa watumishi na wadau mbalimbali wa Usafiri wa Anga ikiwa na lengo la kuhimarisha afya zao na kuwaleta pamoja.

Miongoni mwa Taasisi zilizoshiriki mbio hizo ni Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Shirika la Ndege la Tanzania(ATCL), Shirika la ndege la Precision pamoja na wadau mbalimbali wa Usarifi wa Anga hapa nchini.

Akizungumza kwenye Mbio hizo Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Ng'wilabuzu Ndwata Ludigija amesema ameshiriki kwenye mbio hizo ili kuhamasisha wakazi wa Wilaya ya Ilala kufanya mazoezi kwani maozezi yanaleta afya ya Akili na mwili.

Ili kuepukana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza kama vile Presha na Kisukari Serikali inahamasisha watu kufanya mazoezi ili kuweza kupunguza matatizo mbalimbali kwenye jamii ya kiafya hasa kwa watumishi ambao wanatumia muda mwingi kukaa kwenye ofisi na pamoja na kwenye magari wanakosa muda wa kufaya mazoezi alisema Ludigija.

Amesema kuelekea miaka 60 ya Uhuru na maadhimisho ya miaka 70 ya Usafiri wa Anga ni vyema kama mkuu wa wilaya kuungana nao ili kuhakikisha kwamba wanaunga juhudi na viongozi wakuu wanaohamasisha kufanya mazoezi ya mwili na akili ikiwa ni sehemu pia ya kuwakutanisha watumishi pamoja.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Hamza Johari amesema leo ni siku ya kufanya mbio za wanaanga ikiwa ni kuhadhimisha wiki kimataifa ya Usafiri wa Anga Duniani itayofikia kilele chake tarehe 07 Desemba 2021.

Johari amesema mbio hizi ni kwa ajili ya kujihimarisha kiafya na zilikuwa niza kilomita 5 pamoja na kilomita 10 hivyo watumishi pamoja na wadau mbalimbali wa Usafiri wa Anga wamejumuhika ili kuweka afya zao vizuri.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Hamza Johari akikata upepo
Baadhi ya washirikiri kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Mamlaka ya viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Shirika la Ndege la Tanzania(ATCL), Shirika la ndege la Precision pamoja na wadau mbalimbali wa Usarifi wa Anga hapa nchini wakiwa kwenye mbio hizo.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Ng'wilabuzu Ndwata Ludigija akiwavalisha medali baadhi ya washiriki wa Mbio za kujifurahisha (FunRun) zilizoandaliwa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) na kuwashirikisha wadau mbalimbali wa Usafiri wa Anga hapa nchini.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Hamza S. Johari akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Mbio za kujifurahisha(FunRun) zilivyowakutanisha wadau mbalimbali wa usafiri wa Anga wakati wa maadhimisho ya wiki ya kimataifa ya Usafiri wa Anga Duniani inayofia kilele tarehe 07 Novemba mwaka 2021. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Ng'wilabuzu Ndwata Ludigija
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Ng'wilabuzu Ndwata Ludigija akizungumza na waandishi wa habari kuhusu namna serikali inavyoshirikiana na taasisi kuhamasisha kufanya mazoezi alipofika kushiriki Mbio za kujifurahisha(FunRun) zilizoandaliwa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA).
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Hamza S. Johari akizungumza na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Mamlaka ya viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Shirika la Ndege la Tanzania(ATCL), Shirika la ndege la Precision pamoja na wadau mbalimbali wa Usarifi wa Anga hapa nchini mara baada ya kumalizika kwa mbio za kujifurahisha(FunRun).
Wafanyakazi wa Shirika la ndege la Precision wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kumaliza mbio za kujifurahisha(FunRun) zilizoandaliwa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) na kuwashirikisha wadau mbalimbali wa Usafiri wa Anga hapa nchini.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Hamza S. Johari akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa Mamlaka ya viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) mara baada ya kumaliza mbio za kujifurahisha(FunRun) zilizoandaliwa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) na kuwashirikisha wadau mbalimbali wa Usafiri wa Anga hapa nchini.
Furaha baada ya kumaliza mbio
Mazoezi ya viungo yakiendelea
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: