Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Msaada wa Kisheria kwa Wanawake na Watoto ( WLAC) Theodosia Muhulo, akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani baada ya ufunguzi wa kongamano la kujadili namna ya kukomesha vitendo vya ukatili kwa watoto. Kongamano hilo limeandaliwa na Kituo cha Msaada wa Kisheria kwa Wanawake na Watoro ( WLAC) ikiwa ni siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.
Kamanda wa polisi Kanda Maalumu Dar es Salaam Jumanne Muliro akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani baada ya ufunguzi wa kongamano la kujadili namna ya kukomesha vitendo vya ukatili kwa watoto. Kongamano hilo limeandaliwa na Kituo cha Msaada wa Kisheria kwa Wanawake na Watoro ( WLAC) ikiwa ni siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.
Maofisa wa jeshi la polisi wakiwa katika Picha ya pamoja na wadau wa kupinga ukatili wa kijinsia kwa watoto wa kike wakati wa kongamano la kujadili namna ya kukomesha vitendo vya ukatili kwa watoto. Kongamano hilo limeandaliwa na Kituo cha Msaada wa Kisheria kwa Wanawake na Watoro ( WLAC) ikiwa ni siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.
Wafanyakazi wa Kituo cha Msaada wa Kisheria kwa Wanawake na Watoto ( WLAC) wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa kongamano hilo.
KAMANDA wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema licha ya kupiga vita vitendo vya watoto kufanyiwa ukatili wa kijinsia lakini vitendo hivyo bado vipo sana na vinazidi kuendelea kila kukicha.
Amesema, pamoja na jitihada ambazo zinafanywa na wadau mbalimbali wakiwamo WLAC, wanasheria na Jeshi la Polisi kupambana na vitendo hivyo, lakini bado watoto wa wanaendelea kufanyiwa ukatili wa namna mbali mbali ikiwemo wa kijinsia.
Kamanda Muliro alisema hayo leo Desemba 7, 2021 katika kongamano la kujadili namna ya kukomesha vitendo vya ukatili lililoandaliwa na Kituo cha Msaada wa Kisheria kwa Wanawake na Watoto(WLAC) ikiwa ni mwendelezo wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.
Amesema, wadau mbali mbali, WLAC, wanasheria na Jeshi la Polisi kupitia dawati la jinsia, wanafanya juhudi kubwa kumaliza vitendo hivyo... "wote hao wamekuwa wakielimisha sana na kupambana na vitendo hivi vya ukatili hasa vinavyoendelea kufanywa kwa watoto, lakini bado hawasikii wanaendelea kushupaza shingo na kuwakatili watoto, " amesema.
Amesema kufuatia hali hiyo jeshi la polisi halitosita kumchukilia sheria mtu yeyote atakayebainika kufanya vitendo hivi si kwa watoto tu bali kwa mtu yeyote kwani yeyote anayefanya haya ni mhalifu na ninatangaza kiama kwai pindi tu wakikamatwa.
sasa nasema hivi, niko tayari kumtia mtu kwenye tanuri la kisheria, yeyote anaendelea kuendekeza vitendo hivi, hatabaki salama,”amesema Muliro.
Amesema, huu si wakati wa kumuona mtu Huruma kwa sababu hawa watu wanatuharibia watoto na ambao ndio viongoni wajao, wanatengeneza taifa ambalo limeharibiwa, na kwa namna hii siko tayari kuendelea kuvumilia waharifu wa namna hii kama ambavyo sijawahi kumvumilia mharifu yeyote, lazima wakutane na tanuri la sheria na nitasimamia kwa nguvu zote muongozo wa kisheria kuhakikisha kwamba wanawajibishwa.” amesema.
Aidha Muliro amewaomba wananchi kushirikiana na jeshi la polisi katika kuwabaini watuhumiwa wanawafanyia vitendo hivyo vya ukatili watoto ili kuhakikisha wanavikomesha na kujenga watoto walio bora na siyo walioharibiwa.
“Hatuwezi kutarajia kupata miujiza ya kuwa na watotyo wazuri kwenye jamii wakati sisi wenyewe ndiyo tunaanza kuwajengea ubaya kuanzia kwenye familia, hakuna mtoto ambaye anaweza kuwa bora kwenye jamii wakati ubora huo hakuonyeshwa tangia mwanzo, hatuwezi kukubali hali hii iendelee,”alisema Muliro.
Kwa upande wake, Mkuu wa dawati la Jinsia Kanda hiyo, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, Leah Mbunda, amesema ukatili unaongoza kufanyiwa watoto hao ni wa ulawiti, ubakaji pamoja na vipigo.
Amesema sababu kubwa ya kuendelea kuwapo kwa vitendo hivi ni mmomonyoko wa maadili, Wazazi na walezi wamekuwa na mbio nyingi za kutafuta maisha, hiyo ni sawa lakini katika mbio hizo inapelekea watoto kukosa huduma, watoto wanajilea wenyewe kuanzia muda wa kwenda shule hadi kulala.
Amesema, wazazi wanarudi na kukuta mtoto akiwa amelala, changamoto nyingi amezipata hapo kati kati lakini hakuna mahali alipoweza kushtaki hivyo wanakosa haki ya kusililzwa.
Amesema miongoni mwa wanaowafanyia watoto vitendo hivyo ni watu waliokaribu nao wakiwamo wazazi, ndugu na wale ambao wamekuwa wakiaminiwa au kuwa karibu zaidi na watoto hao.
Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa WLAC, Theodosia Muhulo, amesema changamoto kubwa iliyo katika kushughulikia mashauri yanayohusu ukatili huo ni kukosa ushirikiano wa ushahidi kutoka kwa wazazi, walezi na wale ambao wanaripoti vitendo hivyo hususani wanapofanya michakato ya kuwafikisha watuhumiwa katika vyombo vya dola.
“Tatizo kubwa linalokwamisha mapambano dhidi ya vitendo hivi ni kukosa ushirikiano kutoka kwa ndugu iwe wazazi, walezi au wale wanaoshuhudia na kutoa taarifa juu ya vitendo hivi, mwanzoni huwa wanatoa ushirikiano mzuri, lakini mnapoanza mchakato wa kufikisha kwenye vyombo vya dola kuanzia kwenda polisi hadi mahakamani, huwa wanakimbia na kwenda kumalizana na watuhumiwa ,”amesema Muhulo.
Toa Maoni Yako:
0 comments: