Na Khadija Kalili Kibaha
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Alhaj Abubakar Kunenge amesema mwaka huu kuna mabadiliko makubwa kwa zao la Korosho kutokana na ubora wake ikilinganishwa na ilivyokuwa mwaka Jana.
"Mwaka jana Mkoa wa Pwani ulikua na changamoto ya kuzalisha Korosho zenye ubora wa daraja la kwanza tofauti na ilivyo kwa mwaka huu ambapo bei ya wastani ilikua 1300 kwa kilo moja kwa Korosho za daraja la kwanza lakini mwaka huu bei imepanda hadi kilo moja imenunuliwa kwa Sh. 2,400 hivyo imekua ni faida kwa mkulima.
RC Kunenge alisema hayo leo alipokuwa alifanya ziara ya kutembelea viwanda vinavyobangua Korosho vilivyopo Wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani.
Akiwa katika Kiwanda Cha Tera Cashew nuts kilichopo eneo la Tanita Kibaha alisema kuwa Mkoa utahakikisha matarajio ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan yanafikiwa kwa kubangua Korosho ndani ya Mkoa wa Pwani ambapo ubanguaji utafanyika kwa njia za kisasa kiwandani hapo.
"Tutahakikisha Korosho zote zinakuja kubanguliwa Mkoa wa Pwani na hata zinazotoka nje ya Mkoa huu tutahakikish tunafikia hili tamanio la Mheshimiwa Rais alilolisema hivi karibuni kuwa anataka kuona Korosho zinabanguliwa ndani ya Mkoa wetu tutatimiza hilo kwa ufanisi mkubwa kwani hivi Sasa ubora wa korosho umeongezeka"alisema RC Kunenge
Aidha mbali ya Kiwanda Cha Tera Cashew nuts pia alitembelea Kiwanda Uvuki kilichopo Visiga Kibaha.
"Tumetembea Ili kuona uwezo wa ubanguaji wa zao la Korosho ambapo Tera Cashew nuts uwezo wao ni mkubwa katika kubangua Korosho na kuzikausha Kisasa zaidi ambapo hubangua na kusindika tani 3000 kwa mwaka na pia wamesema kuwa wanatarajia kuleta mashine nyingine mpya ambapo kwa siku watakuwa na uwezo wa kuzalisha tani 7 na kwa mwezi watazalisha tani zaidi ya 200, kama mlivyoona kuwa kiwanda Tera Cashew nuts ni Kiwanda kikubwa cha ubanguaji korosho katika Mkoa wa Pwani na nchini kwa ujumla.
Meneja wa Kiwanda hicho Chiraq Patel alisema kuwa Tera Cashew nuts wanauza Korosho katika soko la nje huku alizitaja baadhi ya nchi wanazouza kuwa ni Morocco, Ethiopia, Hispania
Mwaka jana Mkoa wa Pwani ulizalisha tani 7,000 tu na mwaka huu tayari asilimia 77 ya Korosho ni nidaraja la kwanza hivyo zimeongezeka ubora wake.
Toa Maoni Yako:
0 comments: