Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani Wilbroad Mutafungwa akizungumza na Madereva katika Kituo Kikuu cha Mabasi Magufuli jijini Dar es Salaam.
Mkaguzi wa Mabasi Kituo Kikuu cha Mabasi cha Magufuli Ibrahimu Samwix akiwaonesha madereva wa mabasi miguu ya tayari 'Bolt Joint' walizozitoa kwenye mabasi yao kuwa na ubovu ,jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani Wilbroad (kulia) Mutafungwa akipata maelezo ya vifaa vilivyotolew a kwenye mabasi vikiwa vibovu kutoka kwa Mkaguzi Kituo cha Mabasi cha Magufuli Ibrahim Samwix (kushoto.)
Baadhi ya madereva wakiwasikiliza maelekezo kutoka Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani.

* Samwix asema wenye mabasi mabovu wajiandae kisaikolojia kamwe safari hawatasifanya

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV

KAMANDA wa Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani Wilbroad Mutafungwa amesema kuwa kuna baadhi ya Wamiliki wa Mabasi kwa mabasi yanayoenda zaidi ya masaa Nane wamekuwa wakiweka dereva wa pili asiye na sifa na kusababisha basi kuendeshwa na dereva mmoja kwa safari zaidi ya masaa hayo.

Amesema kuwa wakati wa ukaguzi na utoaji elimu katika Kituo cha Mabasi ya mikoani na nje ya nchi Magufuli, Mutafungwa amesema kuwa katika kulinda usalama wa abiria atakula sahani moja na wamiliki wenye tabia hiyo kwani wanahatarisha maisha abiria.

Amesema kuwa jitihada zilizopo ni kukubaliana na madereva kufuta ajali barabarani ikiwa ni pamoja na baadhi ya madereva wamekuwa wakizingatia sheria za usalama barabarani .

Aidha amesema kuwa kuna dereva wa Kampuni ya BM alipigwa taa na kufungiwa miezi mitatu ambapo alikwenda Kamanda wa Polisi kudai kuwa ameonewa na kuangalia upya na kuona makosa ambapo ameongeza kufungiwa leseni yake miezi mitano.

Amesema wamejipanga kwani kwa wale wenye makosa hakuna ambaye atatoka salama kutokana na elimu inayotolewa lakini baadhi wanakwenda tofauti na elimu hiyo.

Katika ukaguzi uliofanyika mabasi 18 kwa Desemba 10,2021 wamezuia kufanya safari mpaka pale watapokuwa wamejiridhisha kuwa ni salama kwa kufanya safari.

kwa Upande wa Mrakibu Jeshi Polisi na Mkaguzi wa Kituo cha Mabasi Magufuli Ibrahim Samwix amesema kuwa hakuna basi litaloondoka katika kituo hicho likiwa lina ubovu.

Samwix amesema kuwa na madereva wanaoamini mabasi yao mabovu watowe taarifa kwani wakipakia abiria wajiandae kisaikolojia kuwa hawatakweda safari hiyo.

Hata hivyo amesema kwa elimu wanayotoa ni endelevu na sio kwa ajili ya mwisho wa mwaka kwani vyombo hivyo viko mwaka mzima.

Samwix Amesema makosa ya kibidamu yote ni uzembe pamoja na ubovu wa mabasi ni uzembe wa mafundi wa mabasi hayo na madereva wanashindwa kusema kutokana na kukosa posho.

Hata hivyo amesema baadhi ya wamiliki kuwafuta kazi madereva kwa sababu ya kusema mabasi yao mabovu hivyo kazi kwetu kufuta hizi tabia kwani akipewa dereva mwingine naye hataweza kufanya safari.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: