NA PATRICIA KIMELEMETA

BAADHI ya watoto njiti ambao wanazaliwa wakati figo zao hazijakomaa, wana uwezekano mkubwa wa kupata matatizo ya figo wakiwa wakubwa.

Akizungumza na Mwandishi wa Habari hii jana, Daktari Bingwa wa magonjwa ya watoto, Francis Furia alisema kuwa, watoto hao wanahitaji uangalizi wa hali ya juu kuanzia tumboni kwa mama zao hadi wanapozaliwa ili waweze kupatiwa matibabu.

Alisema kuwa, baadhi yao wanazaliwa wakiwa wanashindwa kupumua na wengine wanapata malaria, hali ambayo inasababisha kupata matatizo ya figo, hivyo basi wazazi na walezi wanapaswa kuwa makini kuanzia wanapopata mimba hadi wanapojifungua ili kuhakikisha mtoto hazaliwi akiwa njiti, Bali wanazaliwa wakiwa na uzito unaohitajika.

"Baadhi ya watoto wanazaliwa njiti figo zao zinakua hazijakomaa vizuri, hali ambayo inaweza kusababisha kupata magonjwa ya figo wakiwa watu wazima hadi umri wa miaka 40," alisema.

Aliongeza kuwa, mzazi anapojifungua mtoto njiti, wanapaswa kuzingatia ushauri unaotolewa na watalaam wa afya ili kumkinga na magonjwa mbalimbali yakiwamo malaria na shinikizo la damu, hali ambayo husaidia kupunguza tatizo.

Alisema kuwa, kwa sasa hospitali ya Taifa ya Muhimbili imeanza matibabu ya kupima watoto kuanzia tumbonj mwa mama zao ili kuangalia ukuaji wake na mifumo ya damu na mkono hali ambayo jnasaidia kugundua tatizo wakiwa tumboni, ili waweze kumuangalia mjamzito kwa umakini mpaka atakapojifungua.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: