Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe kuzindua Mwongozo wa Kushughulikia Ukatili wa Kijinsia katika Vyuo Vikuu na Vyuo vya Kati nchini, kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, Novemba 25, 2021. Kushoto ni Naibu Waziri wa Afya, Maendelo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mwanaidi Ali Khamisi na kulia ni Wakili Anna Kulaya ambaye ni Mratibu wa Shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo.
Mratibu wa Ukatili wa Kampeni ya Siku 16 ya kupinga Ukatili wa Kijinsia Wakili Anna Kulaya akizungumza wa uzinduzi wa kampeni iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo Novemba 25, 2021.

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV

SHIRIKA la Wanawake katika sheria na Maendeleo Afrika WilDAF chini ya Mratibu wa Kampeni Siku 16 za ukatili dhidi ya Wanawake Kitaifa Anna Kulaya amesema Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Hassan Suluhu ameiongoza Serikali yake kwa jitihada za dhati za kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia na kuhakikisha vinatokomezwa kabisa.

Amesema kuwa ukomeshwaji huo unawezesha wanawake na mabinti kushiriki kwenye shughuli za maendeleo na kwamba kwa mwaka huu kumeazishwa Mahakama maalum ya kushughulikia masuala ya familia ili kuongeza upatikanaji wa haki kwa wakati kwa wanawake na watoto.

Anna ameyasema haya jijini Dar es salaam mbele ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati wa uzinduzi wa kampeni ya siku 16 za uharakati dhidi ya ukatili wa kijinsia ambapo alisema wameipongeza Serikali kwa kuwaruhusu mabinti wanaopata mimba wakiwa masomoni kuendelea na shule baada ya kujifungua.

"MKUKI tunatoa wito kwa Serikali na wadau wote kuongeza jitihada za kukomesha vitendo vya ukatili wa kijinsia ili kuharakasha kufikia lengo kubwa la kupunguza, hivyo kwa asilimia 50 kufikia mwaka 2022 kama ilivyoainishwa na MTAKUWWA, zaidi kumaliza vitendo hivi na kufikia maendeleo endelevu ifikapo mwaka 2030." amesema Anna

Nakuongeza kuwa "Sisi kama wana MKUKI tunaamini kuwa muda sasa umefika kutengeneza kizazi kipya kinachothamini usawa wa kijinsia." alisisitiza

Anna amesema Kauli mbiu ya Mwaka huu kuhusu ukatili wa kijinsia ni'' EWE MWANANCHI KOMESHA UKATILI WA KIJINSIA SASA.'' Kupitia kauli mbiu hiyo wanaiomba Serikali kutunga sheria ya kudhibiti ukatili wa kijinsia ( Gender Based Violence Violence Act) kwani ukosefu wa sheria mahususi ya makosa ya ukatili ni changamoto kubwa katika upatikanaji wa haki kwa watendewa na kuwatia hatiani watuhumiwa.

Pia amesema kuharakishwa kwa mabadiliko ya sheria ya ndoa juu ya mwaka 1971 ili kuokoa mabinti dhidi ya ndoa za utotoni .kuboresha muundo na kutengwa bajeti ya kutosha kwa ajili ya utekelezaji wa mpango kazi wa taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto MTAKUWWA.

Pia amesema kuna umuhimu wa kufuta sheria zote za kibaguzi mathalani sheria ya kimila ya mirathi, tangazo la serikali Namba 436 la mwaka 1963 ambayo inanyima wanawake haki yao ya kikatiba ya kumiliki Mali kupitia urithi.

Anna akizungumzia siku 16 alisema kutakuwa na shughuli mbalimbali na midahalo ili kuleta mabadiliko katika nchi nakwamba shughuli hizo ni pamoja na maonesho ya matumizi ya digitali, kukuza usawa wa kijinsia na utawala bora ,kongamano la kitaifa kujadili ukatili wanaofanyiwa wanawake wenye ulemavu, msafara wa kijinsia (Caravan Route) kuhamasisha uanzishwaji wa madawati ya kushughilikia ukatili.

Amesema kongamano kwa viongozi wa dini kushiriki katika harakati za kukomesha ukatili wa kijinsia na tuzo kwa vinara 16 wa kupinga ukatili wa kijinsia zitatolewa, lakini pia alibainisha kwamba matukio ya ukatili kwa watoto yaliyoripotiwa na jeshi la polisi kati ya kipindi cha januari 2021 hadi septemba 2021 yanaonyesha kuwa watoto 6168 kati yao wasichana 5287 na wavulana 88.

Amefafanua kuwa wamefanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia kati ya hao watoto 3524 walibakwa 637 walilawatiwa 1887 walipata mimba na 130 walichomwa moto na kinachosikitisha zaidi ni kati ya visa vilivyoripotiwa watuhumiwa waliofikishwa mahakamani ni 3800 kesi zilizofanyiwa upelelezi ni 2368 na zilizotolewa hukumu 88.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: