Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akipokea maelezo kutoka kwa meneja chapa wa mamlaka ya bandari ya Singapore bwana Eugene Tay namna banadari hiyo inavyotumia teknolojia katika kurahisisha upakiaji na upakuaji makasha.Novemba 18,2021.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akitazama kupitia chumba maalum zoezi la upakiaji na upakuaji wa mizigo kisasa katika Bandari ya Singapore wakati alipotembelea bandari hiyo . Novemba 18,2021
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akipokea maelezo kutoka Mkuu wa Uhusiano wa Mamlaka ya Bandari ya Singapore Chris Chan kuhusu matumizi ya bandari hiyo kwa kutumia mitambo maalum ya Tehama katika kupakia na kupakua mizigo kwenye meli wakati alipotembelea Bandari hiyo Novemba 18, 2021.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Uhusiano wa Mamlaka ya Bandari ya Singapore Chris Chan wakati alipotembelea Bandari hiyo Novemba 18,2021. Wengine ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Balozi wa Tanzania Nchini India Baraka Luvanda.

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango leo tarehe 18 Novemba 2021 ametembelea Bandari ya nchi ya Singapore na kujionea namna inavyofanya kazi.

Katika ziara hiyo Makamu wa Rais alishuhudia teknolojia mbalimbali zinazotumika katika kufanya kazi katika bandari hiyo ikiwemo upakuaji na upakiaji makasha na mizigo, ukaguzi wa mizigo pamoja na ufuatiliaji makasha wakati wote yanapokMakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango leo tarehe 18 Novemba 2021 ametembelea Bandari ya nchi ya Singapore na kujionea namna inavyofanya kazi.

Katika ziara hiyo Makamu wa Rais alishuhudia teknolojia mbalimbali zinazotumika katika kufanya kazi katika bandari hiyo ikiwemo upakuaji na upakiaji makasha na mizigo, ukaguzi wa mizigo pamoja na ufuatiliaji makasha wakati wote yanapokuwa safarini.

Akitoa maelezo namna bandari hiyo ilivyopiga hatua kubwa katika kipindi cha muda mfupi makamu wa Rais wa Mamlaka ya Bandari ya Singapore anayeshugulikia masuala ya biashara bwana Ong Seow Leong amesema bandari hiyo imewekeza katika mafunzo pamoja na ubunifu uliopelekea kuongezeka kwa teknolojia inayotumika hivi sasa katika kutoa huduma ikiwemo kuweza kufanikiwa kushusha na kupakia makasha laki moja ndani ya siku moja.

Amesema bandari ya Singapore imekua na mtandao na bandari zingine duniani hivyo kuongeza ufanisi wa ufanyaji kazi wa bandari hiyo. Aidha ameongeza kwamba Bandari ya Singapore imekuwa ikiweka mkazo katika kutafuta masoko pamoja na kufanya tafiti zinazoweza kuongeza watumiaji wa bandari hiyo.

Katika hatua nyingine Bwana Leong ameeleza kuwa ni lazima kuwepo na mipango ya muda mrefu katika uendeshaji wa bandari na tayari nchi ya Singapore inaendelea na ujenzi wa bandari mpya na ya kisasa ambayo kwa miaka ijayo itaweza kutoa huduma kwa ufanisi zaidi.

Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango amesema Tanzania itashirikiana na Uongozi wa Bandari ya Singapore katika kutoa mafunzo kwa watumishi wa bandari za Tanzania pamoja na kupeleka watalaamu wa bandari kutoka Singapore kwenda Tanzania ili kushirikiana katika kufanya maboresho ya haraka hasa bandari ya Dar es salaam.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: