Dkt.Fika Mwakabungu Mkurugenzi wa mafunzo na Mitaala kutoka taasisi ya taasisi ya Elimu Tanzania,akizungumza katika kongamano lililoandaliwa na Taasisi ya The foundation for tomorrow juu ya mtazamo mpya wa Elimu
Dkt.Angelista Joseph kutoka katika Chuo kikuu Cha Catholic Mwenge akizungumza katika warsha ya kuwajengea waalimu uwezo Jijini Arusha
Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya The foundation for tomorrow juu ya mtazamo mpya wa Elimu


Mratibu wa mafunzo kwa waalimu,kutoka taasisi ya Foundation fortomorrow Adrean Maganga,akizungumza na waandishi


Mwalimu wa taaluma Mary Shayo kutoka shule ya msingi Elikiurei:Waalimu,wakijengewa uwezo hata kazi kwao unakuwa rahisi maana tunatumia muda mwingi kuwa na wanafunzi n akuwajengea uwezo na ubunifu

Warsha ya kuwajengea waalimu uwezo iliyoandaliwa na Taasisi ya The foundation for tomorrow juu ya mtazamo mpya wa Elimu ikiendelea

Na Vero Ignatus, Arusha

Waalimu wameomba kujengewa uwezo kupitia semina mbalimbali ili kuwasaidia kupata mbinu mbalimbali za kujenga mwanafunzi umahiri pamoja na kuwajengea uelewa na ubunifu

Akizungumza mwalimu wa taaluma Mary Shayo kutoka shule ya msingi Elikiurei:Ni kwamba waaalimu wajengewe uwezotangia mtaala mpya ulioletwa waalimu hawajawahi kuwezeshwa lakini kupitia warsha kama hii waalimu tutapata uwezo wa kuwaelekeza wanafunzi h

Dkt.Fika Mwakabungu ni Mkurugenzi wa mafunzo na Mitaala kutoka taasisi ya taasisi ya Elimu Tanzania ,katika kongamano lililoandaliwa na Taasisi ya The foundation for tomorrow juu yamtazamo mpya wa elimu,kwamba waalimu wanatakiwa kujiongeza katika ufundishaji wa kupambanua vitu

‘’Tunatakiwa kujiongeza kwelikweli katika ufundishaji wetu tupambanue vitu tunjenga watu wa kujiajiri au wa kuajiriwa sasawatoto nao wanakuwa wakali kweli kweli,tuweke vitu ambavyo watavikiri ,watavichambua na kuona viko sawa’’alisema Mwakabungu

Dkt.Mwakabungu alisema kuwa Taasisi ya elimu Tanzania hivi karibuni imekuwa ikikusanya maoni kutoka kwa wadau mbalimbali wa elimu kuhusiana na mitaala iliyopo katika elimu ambayo waalimu wanaitekeleza.

‘’Wathibiti ubora wanakwenda kuangalia je mitaala hii inakwenda kumjenga huyu mtoto ambae tunamtaka ? tulifanya uwasilishaji mkubwa dar es salaam dodoma na Zanzibar,kilichoonekana ni kwamba mitaala nimizuri mno lakini tatizo lipo kwenye utekelezaji ,kwani ni kwa namna gani kunawawezesha waalimu ili waweze nao kuwekeza kwa wanafunzi’’alisema Mwakambungu

Alisema kuwa ni vyema waalimu wakajiuliza ni namna gani wanawafundisha wanafunzi, katika kutengeneza au kukuza ujuzi kwa waalimu ,mafunzo katika mikakati bora ya ufundishaji wasasa,kuanzisha ukosoaji , thamini pamoja na ufundishaji unaomzingatia mwanafunzi na kuleta ubunifu badala ya kukariri.

Kwa upande wake Mratibu wa mafunzo kwa waalimu kutoka taasisi ya Foundation for tomorrow Adrean Maganga alisema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuongeza /kukuza ujuzi kwa waalimu,kutengeneza muungano wa/mtandao wa waalimu Tanzania,uboreshaji wa morali,kwa utambuzi wa kazi ya ualimu na kuridhika kwao kutasababisha hamu ya kujifunza zaidi ,kuipenda kazi yao,hatimae kuelekea muungano wa na ustawi wa kada ya ualimu katika jamii.

Maganga alisema kuwa mafunzo hayo katika mkakati wa wa ufundishaji wa sasa,kuanzisha ukosoaji wa thamani endelevu,tafakuri na kuanzisha michakato ya uboreshaji,utasababisha ufundishaji unaomzingatia mwanafunzi na kuleta ubunifu katika ufundishaji.

‘’Waalimu ambao wanahisi kushikamana hujisikia kuwa na ujasiri na kuthaminiwa jambo ambalo linahimiza waalimu kupata taarifa na rasilimali zaidi na kuongeza tabia ya kushirikiana ‘’alisema Maganga

Malengo ya taasisi hiyo kukuza ujuzi wa waalimu,ikiwa ni pamoja na mafunzo katika mikakati bora ya ufundishaji wa sasa,kuanzisha ukosoaji na thamani endeleu ,tafakari,na kuanzisha michakato ya uboreshaji,ambayo itasababisha ufundishaji unaomzingatia mwanafunzi na kuleta ubunifu katika ufundishaji.

Kutengeneza muungano au mtandao wa waalimu nchini Tanzania,kwasababu waalimu wanaposhikaman hujisikia kuwa na ujasiri,na kuthaminiwa ,hii ni sambamba na uboreshaji wa morali kwa waalimu
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: