Mha.Baba Askofu Raphael Reuben Haule wa kanisa Anglikana Tanzania dayosisi ya Ruvuma akizungumza na waumini wa kanisa hilo katika jubilee ya miaka 50 ya kanisa dayosisi ya Luvuma iliyofanyika Liuli wilayani Nyasa.
Mha.Baba Askofu Raphael Reuben Haule wa kanisa Anglikana Tanzania dayosisi ya Ruvuma akionyesha kiasi cha fedha shilingi miloni moja kilichotolewa kwa ajili ya mfuko maalumu wa maboresho ya hospitali ya mtakatifu Anna.

Lango la hospitali ya mtakatifu Anna iliyopo Liuli wilayani Nyasa mkoani Ruvuma wakati mmoja wa wananchi wa Liuli akiingia kufuata huduma katika hosptali hiyo.

Na Amiri Kilagalila, Njombe

Serikali nchini Tanzania inaombwa kuunga juhudi za kanisa katika kujenga jamii iliyo bora kiafya kwa kuitazama hospitali ya mtakatifu Anna anayomilikiwa na kanisa iliyopo Liuli halmashauri ya wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma kutokana na changamoto mbali mbali ikiwemo uchakavu wa miundombinu,uhaba wa madawa na vifaa tiba pamoja na upungufu wa watumishi wa hospitali hiyo huku ikitegemewa na wakazi wa mwambao wa ziwa Nyasa.

Wito huo umetolewa na Mha.Baba Askofu Raphael Reuben Haule wa kanisa Anglikana Tanzania dayosisi ya Ruvuma kabla ya uzinduzi wa mfuko wa kuboresha huduma ya hospitali hiyo katika Jubilei ya miaka 50 ya kanisa hilo iliyofanyika katika kanisa la msalaba matakatifu Liuli wilayani Nyasa.

“Kutokana na ghalama za uendeshaji wa taasisi zetu hasa hospitali ombi letu kwa serikali kuendelea kuunga juhudi za kanisa katika kujenga jamii iliyo bora kiafya,tunaiomba serikali iitazame hospitali yetu ya mtakatifu Anna kama vile inavyotazama hospitali zake za serikali”alisema Baba Askofu Raphael Haule

Aliongeza kuwa “Sisi tunahitaji mtusaidie madawa kuleta madaktari na kulipa mishara ya hawa madaktari kwasababu kanisa sisi peke yetu hatuwezi.Tunajua serikali inao mzigo wa taasisi zake za afya lakini hii hospitali ya mtakatifu Anna ni sehemu ya wananchi wenu”

Akizungumza mara baada ya uzinduzi wa mfuko huo ulioambatana na uchangiaji wa fedha,Said Omary Mailon ambaye ni mtendaji wa kata ya Liuli kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Nyasa Kanali Thaomas Labani,Amepongeza mpango wa kanisa katika kuzindua mfuko huo wenye lengo la kuisaidia hospitali huku akitoa wito kwa wananchi na waumini wa kanisa hilo kuendelea kujitolea katika michango ili kuboresha hosptali hiyo.

“Kweli ukienda kwenye eneo la hospitali yetu utakuta hali sio nzuri sana lakini kumbe watu tupo na hapa nimeshuhudia naamini tutaijenga hospitali yetu,serikali haina uwezo wa kutoa fedha katika kila eneo lakini kwa umeoja wetu na fikra zetu tukiweza kuchangia hata elfu kumi zitaweza kuchangia kupunguza changamoto za hospitali”alisema Said Omary Mailon

Aidha amesema serikali itaendelea kutoa ushirikiano kwa kanisa ili kufanikisha shughuli zote zinazofanywa kwa lengo la kuwasaidia wananchi wa Nyasa na tarafa ya Liuli kwa ujumla.

Cherls Mbunda ni pandree wa kanisa hilo mtaa wa Wambaguu dinali ya Mbinga na Roda Ndomba ni miongoni mwa waumini wa kanisa hilo walioshiriki katika misa ya jubilee ya miaka 50 ya kanisa na uzinduzi wa mfuko maalum kwa ajili ya koboresha hospitali,wamesema waumini wa kanisa hilo kwa pamoja wamekubaliana kushirika katika mchango ili kusaidia hospitali

“Mapandree wote tumekubali na tumeahidi kuchangia shilingi elfu hamsini kwa mwaka kwa kila Pandree,walei watachangia shilingi elfu tano walei elfu hamsini lakini na watu wa kawaida shilingi elfu tano kwa kila mwaka ili kuboresha hospitali yetu”alisema Mbunda

Aidha waumini wa kanisa hilo wamesema wanaamini michango hiyo itasaidia kwa kiasi kikubwa matatizo yatakayoikabili hospitali huku wakiomba waumini wote na wananchi kuona umuhimu wa mchango huo kwa ustawi wa afya za watu wa Liuli.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: