Mkuranga Forest Adventure Festival ni Tamasha la utalii la kihistoria liliondaliwa na Mhe. Khadija N. Ali Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga kwa kushirikiana na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Ofisi ya Halmshauri ya Wilaya ya Mkuranga pamoja nao 21 Mkuranga Forest Adventure Festival kwa lengo la kuvitangaza vivutio vilivyopo wilayani Mkuranga.

Kwa mara ya kwanza tamasha hilo limefanyika Mkuranga ndani ya Hifadhi ya Mazingira asilia Pugu KaziMzumbwi Safu ya Vikindu ambao upo chini ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kilometa chache kutoka Jijini Dar es Salaam.

Tamasha hilo ambalo lilifanyika kwa muda wa siku mbili liliambatana na mambo mengi ikiwa ni pamoja na usiku wa kufurahi na mambo mengi zaidi yalifanyika siku ya pili ambapo ndio kulikuwa na mambo kibao ikiwa ni pamoja na kukimbia mbio za kujifurahisha KM2,5 na 10 ndani ya Msitu, Kuvuta kamba, kukuna nazi na mengine mengi.
Baadhi ya wakimbiaji wakiwa wanajiandaa kuanza kukimbia ndani ya Hifadhi ya Mazingira asilia Pugu Kazi Mzumbwi Safu ya Vikindu ambapo walikimbia KM 2,5 na 10 yaani kukimbia na kutalii hapo hapo ndani ya Msitu, hapa ndipo mbio zilipo anzia.
Haya ni maeneo mbalimbali ndani ya Msitu wa Vikindu uliochini ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) ambapo pamoja na kukimbia lakini pia ilikuwa ni nafasi yao wakimbiaji kutalii kwa kuwa walikutana na vitumbalimbali ikiwa na pamoja na misitu iliyoshikana nao kukatiza kati yake
Hizi zilikuwa ni mbio za kujifurahisha ambapo wakimbiaji walipofika katika daraja hili la Mikangazi lenye urefu wa mita 52, walitembea wengine kupunga upepo na kuendelea na safari, usipange kukosa kutembelea ni jirani sana na Dar es Salaam
Baada ya kurejea kutoka katika Mbio ambazo zilisindikizwa na kutalii ukafika muda wa kupasha sehemu ya kwanza ambapo pia viongozi mbalimbali wakiongozwa na mwenyeji wao Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mhe.Khadija Ali walipasha, mambo yote haya ni ndani ya msitu wa Vikindu
Msituni kukanoga zaidi baada ya kuanza michezo mbalimbali ukiwepo huu wa kuvuta kamba ambapo kwa wanawake kulikuwa na team Vibonge na team Portable mtenange ulikuwa wa kukata na shoka lakini mshindi alipatikana, usikose kutembelea Msitu wa Vikindu mambo ni mengi
Goma likanoga zaidi wakaja watani wa jadi sasa mashabiki wa Simba na Yanga ambapo mvutano ulikua mkali sana, unazania upande upi ni Yanga na upi ni Simba? Unaona mashabiki wapi walishinda, yote haya ndani ya msitu wa vikindu
Baada ya kupiga mazoezi na michezo ya hapa na pale zikatolewa zawadi kwa wale walioshinda katika mbio za kujifurahisha KM 2, 5 na 10 ambapo Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Abubakary Kunenge aliwavisha nishani za ushindi. Mbio hizo zilikuwa ndani ya Msitu
Baada ya kupata nishani washindi hao walipata picha za hapa na pale na Viongozi Mbalimbali wa Serikali na Mwisho Picha ya Nne viongozi wakapata picha ya Pamoja matata sana, hii yote ilikuwa kunogesha mambo ya Mkuranga Forest Adventure Festival
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mhe. Khadija N. Ali (kulia) akipewa Tuzo na kuvishwa kitu maalum ishara ya kutambua uthubutu wake katika kutangaza utalii katika wilaya ya Mkuranga
Kwa kuwa hili ni Tamasha la kitalii na utamaduni na mambo mengine kibao, hapa Viongozi walipata kupewa zawadi mbalimbali kama zinavyo onekana hapa na vingi vikiwa vimetengenezwa na vijana wajasiliamali, Huko Vikindu msituni kulinoga sana
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mhe. Khadija N. Ali (kulia) alitoa Shahada maalum za pongezi zilizoandaliwa na 21 Mkuranga Adventures kwa wadau mbalimbali ikiwa ni wadau wazuri wa kutangaza utalii wa Mkuranga, walati wa Tamasha la Mkuranga Forest Adventure Festival
Ikaja kutolewa bonge la burudani kutoka katika kikundi kimoja cha ngoma, pamoja na yote walionesha utalaam wao wa kucheza pamoja na kumchezea nyoka aina ya Chatu ambapo kilikuwa kivitio kikubwa yaani utalii na utamaduni
Umahili wa wanawake katika kukuna nazi ukaoneshwa hapa katika kunogesha Tamasha
Wanaume nao wakasema haiwezekani patachimbika nao wakaingia kushindana kukuna nazi, mchuano ukawa mkali sana na mwisho mshindi akapatikana, yote hii ilikuwa ni kunogesha tamasha kubwa la Mkuranga Forest Adventure Festival ndani ya msitu wa Vikindu
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mhe. Khadija N. Ali (kulia) akimkabidhi Fredy Njeje ambaye ni Balozi wa Hiari wa kutangaza utalii wa Tanzania kupitia #Tag yake (#BaloziwaHiariwaUtaliiTz) Shahada ya pongezi iliyotolewa na Taasisi ya 21 Mkuranga Adventures kwa jitihada zake za kuutangaza utalii ndani ya Wilaya ya Mkuranga,wakati wa Tamasha la Mkuranga Forest Adventure Festival.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: