Mkurugenzi Mkuu wa gym ya Herros Gym Fitness Bw. Khalid Faraji akitoa maelezo kwa maafisa wa Wakala wa Vipimo WMA mara baada ya maafisa hao kutembelea gym hiyo kuhakiki vipimo ikiwa leo ni kilele cha maadhimisho ya Siku ya Vipimo Duniani.

Mteja akipima uzito kabla hajaingia katika chumba cha kufanyia mazoezi ya viungo.

Wateja wakifanya mazoezi katika gym ya Herros Gym Fitness Jijini Dar es Salaam.

Maafisa wa Wakala wa Vipimo wakishuhudia namna ya ufanyaji mazoezi katika Gym ya Herros Gym Fitness leo Jijini Dar es Salaam mara baada ya kutembelea gym hiyo kuhakiki vipimo ikiwa leo ni kilele cha maadhimisho ya Siku ya Vipimo Duniani.

mwalimu wa gym ya Herros gym fitness Bw.Eddo Hassan akiwaonesha maafisa wa Wakala wa Vipimo (WMA) namna wateja wanapofika eneo hilo na kufanya mazoezi mara baada ya maafisa hao kutembelea gym hiyo kuhakiki vipimo ikiwa leo ni kilele cha maadhimisho ya Siku ya Vipimo Duniani.

NA EMMANUEL MBATILO

Siku ya leo Mei 20 ambapo ni kilele cha maadhimisho ya Siku ya Vipimo Duniani , Wakala wa Vipimo (WMA) wametembelea sehemu ya kufanyia mazoezi (Gym) katika wilaya ya Kinondoni kuhakiki vipimo katika chuma za kufanyia mazoezi.

Akizungumza mara baada ya kufanya uhakiki katika maeneo hayo Kaimu Meneja WMA mkoa wa Kinondoni Bw.Charles Mavunde amesema wamekuwa wakivihakiki vyuma vya kufanyia mazoezi kwasababu kuyanyua vyuma ambavyo aidha vinauzito mkubwa ama kunyanyua vyuma upande mmoja mdogo na upande mwingine mkubwa kuna uwezekano mkubwa kuleta athari kwa mtumiaji.

"Kila mwaka tumekuwa tukipita katika gym mbalimbali ambazo zipo maeneo yetu kuhakikisha kwamba vile vyuma wanavyovinyanyua vinakuwa uzito uliosahihi na hatimae tunawapa vyeti". Amesema Bw.Mavunde.

Aidha Bw.Mavunde ametoa wito kwa wamiliki wa gym nawananchi kwa ujumla kuhakikisha kwamba wanatumia vyuma ambavyo vinauzito uliosahihi na kuruhusiwa kisheria.

Pamoja na hayo ametoa rai kwa wamiliki wa gym ambao mpaka sasa wanatoa mazoezi kwa wananchi kwa kutumia vyuma ambavyo havijahakikiwa na Wakala wa Vipimo wahakikishe kwamba wanakutana na wakala hao ili kuhakikisha wananchi wanapata mazoezi katika vipimo vinavyokubalika.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa gym ya Herros Gym Fitness Bw. Khalid Faraji amesema mashine zote za kufanyia mazoezi zipo sawa na hakuna malalamiko kutoka kwa wateja wao wanaofika hapo kwaajili ya kufanya mazoezi hivyo ni kutokana na wao kushirikiana na wakala wa vipimo kuhakiki vyuma vya kufanyia mazoezi kila mara.

Nae mwalimu wa gym ya Herros gym fitness Bw.Eddo Hassan amesema kuwa wale ambao wanafanya mazoezi mtaani wanaweza kupata athari mbalimbali ikiwemo kulemaa upande mmoja zaidi ya kwingine.

Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: