Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw. Daudi Kaali, akizungumza kuhusu matengenezo ya Mitambo na Magari yanayotumika katika Kilimo cha umwagiliaji na ujenzi wa miundombinu yake.
Moja ya mtambo katika ofisi za Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Dodoma ukiwa Tayari kukodishwa kwa ajili ya Shuguguli za kilimo cha Umwagiliaji na Ujenzi wa Miundombinu yake.
moja ya gari lililopaki zaidi ya mwaka mmoja aina ya Nissan Diesel lenye namba za Usajili STJ 328, likifanyiwa matengenezo tayari kwa shughuli za umwagiliaji.

baadhi ya Mitambo ambayo ipo katika hatua ya kufanyiwa matengenezo.
Baadhi ya Magari yaliyopo tayari kukodishwa kwa ajili ya shughuli za kilimo cha Umwagiliaji na ujenzi.

NA MWANDISHI WETU, DODOMA

IMEELEZWA kuwa katika robo ya pili ya mwaka wa Serikali,Tume ya Taifa ya Umwagiliaji inategemea na inaendelea kutekeleza majukumu ambayo imepangiwa ikiwa ni pamoja na kutengeneza na kukarabati magari na mitambo iliyokuwa imeharibika na kuacha kufanyakazi kwa muda mrefu, vitendea kazi ambavyo vinatumika katika kuendeleza sekta ya umwagiliaji.

Hayo yamesemwa, na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw. Daudi Kaale, alipokuwa akizungumza Mjini Dodoma, kuhusu ufufuaji na ukarabati wa mitambo inayotumika katika ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya Umwagiliaji.

“tunapojenga Miundombinu ya umwagiliaji tunahitaji mitambo na magari makubwa, Kwa hivyo inafanyika kazi kubwa kwasasa yakufufua vitendea kazi hivyo ili kuweza kujenga uwezo wa Tume na kuendeleza miundombinu ya umwagiliaji.” Alisema Bw. Kaali

Aliendelea kusema kuwa vitendea kazi hivyo ni muhimu sana hasa kwa sasa wakati ambao Tume inakaribia kuanza kutekeleza miradi ya umwagiliaji kwa kupitia force account.

“Miradi hii ambayo inategemea kuanza kutekelezwa kupitia force account inategemea kuanza kutekelezwa mwezi huu hivyo tunahitaji kuwa na vitendea kazi vyakutosha, na mpaka sasa tumeweza kufufua mitambo iliyopo mikoa ya Mbeya ambapo kulikuwa na mitamboa mbayo ilikuwa imeharibika tumeweza kuifufua lakini pia hata hapa makao makuu Dodoma kumekuwa ma mitambomingi, ambayo nayo pia ilikuwa imeharibika ilikuwa haifanyikazi tumeweza kuifufua tumefufua mitambo kama miwili kwa hapa Dodoma katika robo hii ya mwaka, lakini pia tuna maroli matatu,na kule Mbeya tunategemea kufufua eskaveta ambayo ilikuwa imeharibika tunategemea nayo itaanza kufanya kazi.”Alisisitiza

Aidha Bw. Kaali aliongeza kwa kusema kuwa,kwa upande wa mitambo ambayo ufanisi wake umeanza kupungua, nayo itafanyiwa matengenezo yaani,mitambo ambayo imekaa kwa muda mrefu bila kupata matunzo na matengenezo kwa wakati.

“Tunatengemea kumaliza matengenezo hayo ili tuweze kuanza utekelezaji wa miradi ya force account, ambayo tunategemea kuanza mwezihuu.”

Awali, Akizungumza kuhusu swala la kukodisha mitambo kwa taasisi ambazo zinauhitaji, Bw. Kaali ametoa wito kuwa,Tume ya Taifa ya Umwagiliaji inakodisha mitambo ya umwagiliaji na mitambo mizito ya ujenzi kama vile Buldoza na Maroli, kwa wadau mbalimbali kama vile mashirika ya umma, watu Binafsi na taasisi mbalimbali ilikuweza kuchangia katika maendeleo ya nchi huku akieleza vipaumbele vya ukodishawaji wa mitambo hiyo,vinatolewakwa wale wanaofanya shughuli za umwagiliaji wanaotaka kuendeleza skimu zao za umwagiliaji.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: