![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh1LSQF3Mtj9vQpkSQ0kMBmFy1rVyxnljorYuJ6TpNY-fviLoje-0HkgbimnUlioG5546TqLAnUB4H1OhTqpVsgFR8Us5K3xnptxLJLBrCA-iz00SgFFLV8OyBYoEld0WlnmxjqgJPHY-jD/s640/IMGM4148.jpg)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhXv7T0a304UFCxKcZcHZHz5s9r0lNTvOgVp_bQ3jnwvFkKP1bZsmLN_OVIGLEEMbIxKMhIl56TKoJLEoab0pyLOcIb7KgXAMrplNvFSO5ups6pIAzwQ3AFGaVUmDNItRgHP4_EBjmEVXjV/s640/IMGM4123.jpg)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgZe2ud-uHGhuXAkR-tDUbTxEuTQtSkbDXniZiTV3GUoTr5hI2kcIDOzQ7lQnJZBtFa8X5ycW-l17wh0cgfYiQrITF43XxMuIZWM_M5maikMs4SztxsVqTBSzGYsff_rCwwWnzNDt2Yzjz7/s640/IMGM4127.jpg)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjprOo3sQ0PtENJ_YYniiJvXTo_AVzzizu3S7ulQwZTg3c2RnRVDC0SvVqkINNMEoXDCr0SS_4zXu7aijH4GCQTh79DYGl8FYWT3kGUiSltXgle7tZkGc8UFnXlatOI1GwjqEZ9_PY_3RDZ/s640/IMGM4213.jpg)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhElnOSI0Bcs-UOszpm-bu9-HT1UkHESNoz7dxfEzqQYbZrBUG5Pc75Qcv6wTNyhl-QIWexTp3XTo1jAvXnCkQrQO6Mhq4fxB48m7qur2DNRVr4PUdzkwBqZfsh3Pf0fhzt6wartOKRzC5f/s640/IMGM4074.jpg)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEile7RSi0DqSbtehEPdmJcajwulvu6aQmBi0qpen9xiZy9hu5_kRZRxMUEdT3kyCpa_U6ScoOn2A1WiWau0pnsynITTixf2L761as2JWzQ28N9_T34Qu8HkX42jeEBR2DsiVp1p5zlfh5HT/s640/IMGM4258.jpg)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjDaKs9SFdMRm79mmtQh-gi_MFPgWgZb49TD-XEIja2lidLQYvN61XymIwLwyLdhyphenhyphenf6v-r1rIjYA1G-lEFvOkwBkp_q8Mlf838r3-Fqi4q63zhNZyFs1jyASKp04COU_a3UtIkuGzCoZc9N/s640/IMGM4262.jpg)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhWhXiY86KpgftADc_PBwXN8m_HRJUfC_3a3xNzekOP99GLDAU66x7RZ47fZD2abaTJK3MqC8LjvIOJNXQxip8-AqPwH_gmBdN8kiUFzk3uGwmxcpXtKwQ7vpMHX8eaMkLW3oRVlSSCt9p8/s640/IMGM4283.jpg)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhJJt1CqKEPbFZxzhzDoR6LmQKmEtykeyOoIHM-uZvLK_BvEUEUu6xE28ijSngTYz673eHf2T_qZsSscg32Z4aXHQ5eGoq7qAxX-4qGFKtCQ07eSsdz6HRrFKWhd8EXZ5IfG0dJU20lVE70/s640/IMGM4195.jpg)
Na Dixon Busagaga, Arusha.
MAKATIBU wakuu wa Sekta na Maafisa waandamizi wa Wizara zinazo shughulika na Mazingira ,Maliasili na Utalii wamekutana jijini Arusha kwa ajili ya kuweka agenda za Mkutano wa Mawaziri wa sekta husika kwa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo kusini mwa Afrika (SADC) .
Miongoni mwa mambo yanayojadiliwa katika kikao hicho cha awali ni pamoja na mpango mkakati wa pamoja wa kukabiliana na ujangili kwa nchi za SADC ,hoja inayo paswa kuungwa mkono nan chi wanachama.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii ,Prof,Adolf Mkenda amesema nchi moja ni vigumu kupambana na ujangili hivyo tunahitaji kuunganisha nguvu kwa nchi zote ili ziweze kufanikisha juhudi za kupambana na ujangili.
“Tunahitaji kuwa na mpango mkakati wa kukuza utalii katika nchi za SADC, hii ni moja kati ya agenda muhimu zitakazojadiliwa” alisema Profesa Mkenda.
Mkurugenzi wa Idara ya Chakula ,Kilimo na Maliasili kutoka Sekretarieti ya SADC, Domingos Zephania Gove amesema kuwa wanahitaji kutembea pamoja kama nchi za SADC katika kuweka mikakati katika masuala ya Mazingira,Utalii na Wanyamapori .
Gove amesema kuwa wanahitaji kuthibitisha program za pamoja za kukuza utalii na kusimamia maliasili katika ukanda husika.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais ,Muungano na Mazingira,Mhandisi Joseph Malongo amesema kuwa watajadili mkakati wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi kwa pamoja na jinsi ambavyo wananchi wanaweza kutumia uchumi wa bluu kwa maana ya bahari katika kuchangia maendeleo .
Toa Maoni Yako:
0 comments: