Inaelezwa kwamba katika historia za ukombozi wa Viongozi wa nchi za Kusini mwa AFRIKA Wilayani NACHINGWEA mkoani LINDI Pana historia yake.
Nyumba hii iliyopo eneo la "Farm 17" (Samora House ) NACHINGWEA ina historia kubwa. Hapa ndipo Hayati Rais wa Msumbiji SAMORA MACHEL alipofikia na kuweza kupanga mikakati ya kivita dhidi ya Mahasimu wake, wakati huo Makamanda wake wakipata mafunzo kutoka kwa Jeshi lenye weledi la Tanzania.
Hakika nyumba hii ina siri kubwa ya Ukumbozi.
Mikakati ya Uongozi wa Wilaya ya NACHINGWEA ikiongozwa na Mkuu wa wilaya hiyo MH. RUKIA MUWANGO, ni Kuweka mazingira mazuri ya nyumba hii kama kielelezo cha kihistoria, kwa kushirikiana na Ubalozi wa Nchi ya MSUMBIJI hapa Tanzania.
Tutahifadhi kumbukumbu hii kwa Kizazi Cha leo na Kinachokuja.
Mungu ibariki Afrika Mungu ibarika Tanzania.
Toa Maoni Yako:
0 comments: