Mbunge wa jimbo la Kilosa Mbaraka Ba Waziri ametoa msaada wa ujenzi wa kisima kikubwa cha mita 100 ambacho kitakuwa na uwezo wa kuhudumia zaidi ya vijiji viwili katika kijiji cha Rudewa kilichopo kata ya Rudewa wilayani Kilosa ambapo ujenzi wake umeanza mara moja, kutokana na changamoto ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kuwa tatizo sambamba na ahadi ya ujenzi wa kituo cha afya kwaajili ya huduma ikiwemo ya wajawazito pamoja na watoto huku tayari akiwakilisha bati 120 waajili ya ujenzi wa kituo cha afya simenti 200 kwaajili yakujenga vyumba vya madarasa ya shule ya msingi Rudewa katika wilaya ya Kilosa.

Mbunge wa jimbo la Kilosa Mbaraka Ba Waziri akikabidhi diwani wa kata ya Rudewa Subiri Joseph moja ya mfuko wa saruji kama mfano kwaajili ya ujenzi wa madarasa ya shule katika kijiji cha Rudewa Kata ya Rudewa Walayani Kilosa ambapo alitoa msaada wa saruji 200 kwa ajili ya shughuli hiyo.
Mbunge wa jimbo la Kilosa Mbaraka Ba Waziri akimpa mkono diwani wa kata ya Rudewa Subiri Joseph wakati akikabidhi mradi waujenzi wa kisima cha mita 100 kwaajili ya kutatua kero ya maji katika kijiji hicho kulia ni katibu wa CCM wilaya ya Kilosa Aziza Juma kushoto Hassan Mkopi Mwenyekiti wa Halmahauri wilaya ya Kilosa pamoja na viongozi mbalimali wa CCM na serikali.
 Mwenyekiti wa kijiji cha Rudewa Hamad Maboga akipokea bati kutoka kwa diwani wa kata hiyo Subiri Joseph wakati wakikabidhiwa msaada wa vifaa na Mbunge wa Jimbo la Kilosa Mbaraka Ba Waziri kwaajili ya ujenzi wa kituo cha afya katika kijiji hicho.
Mbunge wa Jimbo la Kilosa Mbaraka Ba Waziri akihutubia wakazi wa vijiji na kata ya Rudewa wakati wa mkutano na wananchi hao alipokua akisikiliza kero na kutoa utatuzi wa kero hizo ikiwemo katika sekta ya Afya, Elimu na Maji.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: