Mitandao ya kijamii imesaidia kuwaleta watu pamoja wenye mitizamo inayofanana. Mitizamo ya kisiasa, kiuchumi, kiutamaduni, kimapenzi na hata kifamilia.

Mfano wa mitandao ya kijamii ni Facebook, twiter, whatsapp, instagram, snapchat n.k

Hebu tuangalie baadhi ya hasara za matumizi ya mitandao ya kijamii

Kupoteza muda: Mitandao ya kijamii imewafanya watu wengi kuwa walevi wa hii mitandao. Kundi kubwa ambalo limeathirika ni vijana. Watu wanatumia muda mwingi kuwasiliana mitandaoni na kuwafanya kuwa wazembe sana kufanya shughuli zao za msingi kama vile kazi, kusoma n.k

Kushindwa masomo: Vijana wengi wanaoibukia kwa sasa hasa wenye umri kuanzia miaka 13 kuendelea wako kwenye wakati mgumu sana kuathirika na matumizi ya mitandao ya kijamii na hivyo baadhi kutofanya vizuri katika mitihani yao

Uhalifu: utoaji mwingi wa taarifa za mtu binafsi inaweza kabisa kumfanya mtu kuwa muhanga wa mapenzi au wizi wa fedha na ujangili mbali mbali mitandaoni. Watu wanatumia taarifa hizo kufanya uhalifu.

Kuharibu ama kuchafua sifa binafsi ama za mwengine:Mitandao ya kijamii inaweza kumchafua mtu ama kumkashifu ,ikiwemo kuwekewa picha za utupu ,kuzushiwa jambo ambalo hajalifanya n.k

Udukuzi: Mitandao ya kijamii imewafanya baadhi ya watu kudukuliwa taarifa zao kwa lengo la kufanya uhalifu, kumkomoa ama kutafuta umaarufu.

Matumizi mabaya ya fedha: Hizi ni zile za kununua vifurushi kwa ajili ya kuingia kwenye mitandao ya kijamii na kusahau vipaumbele muhimu.

Migogoro: Mitandao imekuwa ni chanzo kikubwa cha Migogoro ya kifamilia, wapenzi, wanandoa, marafiki na hata kazini.

Maadili yasiyofaa: wapo baadhi ya watu ambao wamekuwa wakiandika ama kupachika mambo ya ovyo, picha mbaya na hata matusi kwenye mitandao. Haya mambo mengi hayazingatii maadili.

Kwa leo tukomee hapa, unaweza pia kutaja zingine. Jiandae pia kuzijua faida za mitandao ya kijamii katika chapisho litalokafuata.

By Jerry Jr. © 2017
Jerry Alfredy Jr.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: