Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza wakati wa ziara ya kutembelea Bandari ya Zanzibar, ikiwa na lengo la kukagua mifumo ya udhibiti wa uingizwaji wa Dawa za Kulevya huku akiliagiza Jeshi la Polisi Zanzibar kushirikiana na Uongozi wa Bandari, kuhakikisha ukaguzi wa mizigo unafanyika ili kukomesha uingiaji wa dawa hizo ambazo humaliza nguvu kazi ya Taifa. Wakwanza kushoto ni Naibu Waziri Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mohamed Ahmada Salum na anayefuatia ni Mkurugenzi Mkuu Bandari ya Zanzibar, Kapteni Mstaafu Abdula Juma. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akitembea kuelekea sehemu inayokaguliwa mizigo wakati wa ziara ya kutembelea Bandari ya Zanzibar, ikiwa na lengo la kukagua mifumo ya udhibiti wa uingizwaji wa Dawa za Kulevya, huku akiliagiza Jeshi la Polisi Zanzibar, kushirikiana na Uongozi wa Bandari kuhakikisha ukaguzi wa mizigo unafanyika ili kukomesha uingiaji wa dawa hizo ambazo humaliza nguvu kazi ya Taifa.Wakwanza kulia ni Naibu Waziri Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Mohamed Ahmada Salum na anayefuatia ni Mkurugenzi Mkuu Bandari ya Zanzibar, Kapteni Mstaafu Abdula Juma. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akikagua jinsi ukaguzi wa mizigo unavyofanyika kupitia komputa wakati wa ziara ya kutembelea Bandari ya Zanzibar ikiwa na lengo la kukagua mifumo ya udhibiti wa uingizwaji wa Dawa za Kulevya, huku akiliagiza Jeshi la Polisi Zanzibar kushirikiana na Uongozi wa Bandari kuhakikisha ukaguzi wa mizigo unafanyika ili kukomesha uingiaji wa dawa hizo ambazo humaliza nguvu kazi ya Taifa. Kulia ni Afisa wa Bandari anayeshughulika na ukaguzi, Adam Masoud. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Mfanyakazi wa kitengo cha mizigo Bandari ya Zanzibar, Saleh Masoud akikagua moja ya mzigo wa abiria wanaoingia kupitia bandari hiyo ambapo Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni,ameliagiza Jeshi la Polisi Zanzibar kushirikiana na Uongozi wa Bandari hiyo kuhakikisha ukaguzi wa mizigo unafanyika ili kukomesha uingiaji wa Dawa za Kulevya ambazo zimekuwa zikiharibu nguvu kazi ya Taifa. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Mkurugenzi Mkuu Bandari ya Zanzibar, Kapteni Mstaafu Abdula Juma (wapili kushoto), akimsikiliza Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, wakati wa ziara ya kutembelea bandari hiyo ikiwa na lengo la kukagua mifumo ya udhibiti wa uingizwaji wa Dawa za Kulevya huku akiliagiza Jeshi la Polisi kushirikiana na Uongozi wa Bandari kuhakikisha ukaguzi wa mizigo unafanyika ili kukomesha uingiaji wa dawa hizo ambazo humaliza nguvu kazi ya Taifa.Wakwanza kushoto ni Naibu Waziri Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mohamed Ahmada Salum na wakwanza kulia ni Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Kifaa cha kubebea kontena kikiwa kimebeba kontena tayari kupelekwa kwenye mashine maalumu ya ukaguzi ambayo hutumia mionzi kukagua mzigo uliopo ndani, ambapo Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni ameliagiza Jeshi la Polisi kushirikiana na Uongozi wa Bandari ya Zanzibar kukagua mizigo yote inayoingia ili kudhibiti uingiaji wa Dawa za Kulevya Visiwani Zanzibar. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.
Toa Maoni Yako:
0 comments: