Katibu wa mbunge jimbo la Isimani Bw Thom Malenga kulia akimkabidhi diwani wa Mboliboli Khalfan Lulimi msaada wa bati kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa miradi ya maendeleo katani kwake msaada huo umetolewa na mbunge Wiliam Lukuvi kwa kata mbali mbali kwa kutoa bati 2000 zenye thamani ya Tsh milioni 44 na Power tila 15 kwa madiwani wote wa CCM jimboni mwake
Diwani wa Mlolo Charles Nyagawa kushoto akikabidhiwa bati na katibu wa mbunge wa Isimani Thom Malenga.
Madiwani wakipokea bati.
Diwani wa kata ya Malenga makali Flanzisca Kalinga akiwa akijiandaa kuendesha moja kati ya Power tila 15 zenye thamani ya Tsh milioni 105 zilizotolewa na mbunge wa jimbo la Isimani mkoani Iringa Wiliam Lukuvi kwa ajili ya madiwani wote 15 wa CCM jimboni mwake kama miradi yao pamoja na bati 2000 zenye thamani ya Tsh milioni 44 kwa ajili ya kukamilisha miradi ya maendeleo jimboni humu wa tatu kushoto ni katibu wa mbunge Lukuvi , Thom Malenga ambae alikabidhi kwa niaba ya mbunge Lukuvi akiwa na baadhi ya madiwani hao.
Na MatukiodaimaBlog
MBUNGE wa jimbo la Isimani Wiliam Lukuvi aametoa msaada wa bati 2000 ajili ya kukamilisha miradi ya kimaendeleo katika kata mbali mbali za jimbo hilo pamoja na kuwasaidia madiwani wote 15 wa chama cha mapinduzi (CCM) Power Tila vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya Tsh milioni 100.44
Lukuvi alisema amelazimika kukabidhi msaada huo wa power tila kwa madiwani wake ili kuwawezesha kiuchumi pia kusaidia kusukuma maendeleo katika kata zao kama kuwasaidia wananchi kutumia power tila hizo kuendeshea shughuli mbali mbali za kijamii zikiwemo za kilimo.
Kwani alisema kuwa power Tila hizo amezinunua zikiwa na kamili ya vifaa vyake vyote kama jembe la kulimia pamoja na tela zake kwa ajili ya kusafirishia mazao ama kufanyia shughuli nyingine za kijamii katika kata.
Akikabidhi msaada huo leo kwa niaba ya mbunge Lukuvi katibu wake Thom Malenga alisema kuwa kuwa lengo la msaada huo ni kusukuma mbele maendeleo ya wananchi wa jimbo la Isimani na kuwa msaada wa bati unakwenda katika kata zote ambazo zina miradi ya ujenzi wa shule, nyumba za walimu na zahanati ambazo zilikuwa zikihitaji bati ili kumalizia ujenzi huo na kuwa bati zote ziliotolewa ni 2000 zenye thamani ya Tsh milioni 44
Wakati msaada huo wa power Tila umeelekezwa kwa madiwani 15 wa CCM waliopo katika jimbo hilo na kuwa kila power tila moja imegharimu kiasi cha Tsh milioni 7 na kwa powertila zote zimegharimu Tsh milioni 105 lengo kubwa la kutoa msaada huo ni kuwawezesha madiwani hao kuwa na vitega uchumi na kuongeza ari ya kuwatumikia wananchi wao.
Toa Maoni Yako:
0 comments: