Muuza mishikaki maarufu Said Mishikaki maeneo ya Stendi ya Temeke jijini Dar es Salaam amejikuta katika wakati mgumu baada ya kupewa kichapo kikali na wananchi waliomkamata akiandaa paka baada ya kumchinja kwa ajili ya kuchoma mishikaki.
Wakizungumza wakazi wa Temeke walisema kuwa jamaa huyo alipewa kichapo baada ya fununu za muda mrefu kuwa jamaa huyo amekuwa akitengeneza mishikaki ya paka.
"Kuna watu wamekuwa wakimsema ila leo imedhihilika na ukweli umefahamika kumbe kila siku analisha watu mishikaki ya paka... ama kweli duniani kuna mambo," Walisema wananchi hao baada ya kumpa kichapo jamaa huyo.
Mchongo wa kumkamata uliwezeshwa na wananchi hao baada ya kutokea nyumbani kwake ambapo alikuwa katika harakati za kuandaa kitowewo hicho tayari kwenda kukichoma barabarani.
Paka akiwa amechinjwa ili kuandaliwa kwa ajili ya mishikaki.
Toa Maoni Yako:
0 comments: