Na Chalila Kibuda

Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa kutumia teknolojia ya uchukuaji wa alama za vidole (BVR) kwa mji mdogo wa Makambako mkoani Njombe utaanza Februari 23 hadi Machi 1 mwaka huu.

Kwa taarifa iliyotolewa katika vyombo vya habari na Ruth Masham kwa niaba ya Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi ya Taifa (NEC) ilisema zoezi hilo litapita katika kata za Kitisi, Kivavi, Lyamkena, Maguvani, Majengo ,Makambako ,Mji Mwema, Mlowa,na Mwembetogwa na zoezi hilo litaanza majira ya saa 2 hadi majira ya saa 12 jioni.

Ruth katika taarifa yake ilidai kuwa Kata ya Kitandililo zoezi la uboresha la daftari la wapiga kura utafanyika Machi 3 hadi 9 na Kata ya Mahongole Machi 11 hadi 17  pamoja na Kata ya Utengule utafanyika Mach 19 hadi 25 na vituo vya kujiandikisha vitakuwa kwenye Vitongoji ,Vijiji na Mitaa.

Watakaohusika katika zoezi hilo ni wale ambao wametimiza miaka 18 na kuendelea na wale watakaotimiza miaka ifikapo Oktoba mwaka huu,waliojiandikisha kwenye daftari la zamani wanatakiwa kuhuisha taarifa zao na kupata kadi mpya za kupigia kura.

Wananchi wote wanatakiwa kujitokeza kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura ili kuwezesha kupiga kura ya Maoni ya Katiba inayopendekezwa pamoja na Kuchagua Viongozi ambao ni Rais,Mbunge pamoja na Diwani.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: