WASOMAJI na wadau wangu nawasalimu na naimani kuwa Mwenyezi Mungu ametujalia tumeuona mwaka mpya wa 2015 salama salmini. Nawatakia heri na fanaka katika mwaka huu pia na karibuni tena katika porojo zangu za ukweli.
IDARA ya Habari –MAELEZO ndiyo idara ya serikali inayoshughulika na kufanya kazi zake kama chombo cha usimamizi wa vyombo vya habari na waandishi wake.
Idara hiyo pia ndio msemaji wa masuala mbalimbali ya serikali lakini pia ndiyo idara yenye jukumu la kusajili au hata kuyafutia usajili magazeti hapa nchini na vyombo mbali mbali vya hjabari.
Waandishi wa habari waajiriwa na wale wa kujitegemea wameanza mchakato wa kujaza fomu kwaajili ya kupatiwa vitambulisho vipya vya kazi (PRESS CARD) kwa mwaka 2015.
Jambo hili ni zuri kwa waandishi wa habari maana kitambulisho hicho cha serikali hutolewa kwa waandishi walio na sifa za uandishi tu na sio wale waparamia fani za watu maarufu kama kanjanja.
Ndio! Uandishi wa habari ni taaluma kama taaluma nyingine, kwa hiyo kila mwanahabari anatakiwa kuwa na Press Card ambacho ndicho kitambulisho cha serikali, kama huna basi wewe sio muandishi au laa hujakomaa kuwa muandishi. SOMA ZAIDI FATHER KIDEVU BLOG
Toa Maoni Yako:
0 comments: