Wengi tunafahamu kuwa Mithali 31: 10-29 imeeleza sifa za mke mwema. Wasichojua wengi kuwa sehemu kubwa ya sifa zinazotajwa kwa mke mwema zinahusu tabia za kiujasiriamali. nafahamika kuwa tunaposema ujasiriamali (au biashara) tunahusisha maeneo yafuatayo: Uzalishaji, Usambazaji na Masoko , Uhasibu, Uchumi na Uwekezaji , Usimamizi wa rasilimali watu na Usaidizi kwa Jamii. Hebu angalia Biblia inavyompamba mke mwema kwa sifa hizi:

1. UZALISHAJI (PRODUCTION)
Anajiishughuisha na uzalishaji kwa kusokota, kufuma na kushona mazulia, mishipi na mavazi kwa kutumia malighafi ya sufu. Mith 31: 13, 19, 22

2. USAMBAZAJI NA MASOKO (MARKETING & DISTRIBUTION).
Akishazalisha bidhaa zake anatafuta mahali kwenye masoko na kuzisambaza, “Huwapa wafanyabiashara mishipi/mavazi yaliyotengenezwa” Mithali 31: 24(b) 

3. UHASIBU (FINANCE)
Biashara yeyote lazima iambatane na mahesabu. Ni lazima ujue gharama unazotumia kuzalisha ili kujua uuze kwa bei gani itakayokuletea faida. Mke mwema ni mwerevu katika hili kwa sababu, Mith 31: 18(b) inasema, “Huona kama bidhaa yake ina faida;…”

4. UCHUMI NA UWEKEZAJI (INVESTING & ECONOMICS TRENDS)
Akishapata faida tunaambiwa mke mwema habweteki, bali ile faida ya biasharani huwekeza katika vitega uchumi vinavyopanda thamani, kama mashamba na mazao ya biashara. Mith 31:16, “Hutafuta shamba akalinunua……..na hupanda mizabibu”

5. USIMAMIZI NA UTAWALA RASILIMALI WATU
(Human Resource Management) Mke mwema wakati wote huhakikisha anaratibu
na kuwasimamia wafanyakazi na watu wa nyumbani mwake kiukamilifu; kwa kuhakikisha anawapa mahitaji yote ya msingi na ziada. Mith 31: 15, 21.

6. KURUDISHA FAIDA KWA JAMII (COORPORATE SOCIAL RESPONSIBILITY)
Kitaalamu biashara zinatakiwa kuzijali jamii zinayozizunguka kwa kurudisha sehemu ya faida kwa jamii. Mke mwema analijua hili kwa sababu tunaambiwa katika Mith 31: 20, “Huwakunjulia masikini mikono yake… huwanyooshea wahitaji mikono yake…”. Ingawa nimezipanga sifa hizi kitaalamu, simaanishi kuwa mke mwema ni yule mfanyabiashara “pure” ama ni yule aliesoma masomo ya biashara, la hasha! Lakini mke mwema Biblia inaonesha kuwa ni lazima awe na mtazamo wa kiujasiriamali-kwa maana ya fikra za kujiongezea kipato. Pengine wale mabinti na wanawake wanaopenda vya mteremko na vya kupewa ama kuhongwa-hongwa ovyo wanaweza
kujitambua kuwa “they are not wife materials”.

Wife material/mke mwema siku zote ni mtafutajina mchakarikaji iwe ameajiriwa, iwe amejiajiri au hata awe mama wa nyumbani!

MWL.CONRAD C
(PROFESA MTOTO)
0753 391634
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: