Ni majira ya saa 2 asubuhi nikitoka zangu Dodoma kwenye usaili narudi zangu Dar ninapoishi. Kutokana na ugumu wa maisha, nimebakiwa na shilingi 3,000 tu mfukoni hapo nikiwaza chakula cha jioni pamoja na nauli ya daladala..tena ukizingatia Mbagala ilivyo mbali.. Nikajipa moyo siku itapita.

Tulipofika Chalinze, basi lilisimama na akapanda mrembo mmoja matata sana, umri kati ya miaka 24 hadi 26, mwenye urefu wa wastani, mweupe, mwembamba kiasi huku akiwa ametupia suruali ya jinsi pamoja na t-shirt iliyomkaa vizuri na kuonesha umbo lake maridhawa la namba nane. Akaja akaketi kwenye siti iliyopo pembeni mwangu kwa kuwa kabla ya kufika chalinze, abiria aliyekuwa amekaa jirani yangu alishuka.. Basi tukasalimiana na safari ikaendelea.

Akajitambulisha anaitwa Angel.. Mimi nikamwambia naitwa Kidevu. Basi tukapiga stori nyingi sana.. Tulipokaribia kufika Mbezi akaniaga akasema atashuka kituo cha Mbezi mwisho kwani ndipo anapoishi. Basi nikamuaga.. tukabadilishana namba za simu.. Kwa kweli alikuwa mcheshi sana na nilifurahi mno kupata namba zake.. Basi baada ya kufika Ubungo wakati natoa mizigo yangu sehemu ya kuhifadhia, nikaona pochi ya kike.

Nikakumbuka Angel nae aliweka mizigo yake pale... nikasema hebu nifungue niangalie ndani... Heeeeh nikakuta pesa nyingi sana za kitanzania pamoja na Dola za marekani nyingi sana pamoja na vitambulisho vya angel.. Nikajiuliza, je nimpigie au nipotezee nisepe na mkwanja?? Wakati nawaza hayo ghafla nikaona simu inaita.. Jina ni Angel... Dah...nikawazaaa huku inaita..nikaamua tu kupokea,

"Hallo, samahani Kidevu eti umeona pochi yangu hapo hata sijui nimeipoteza wapi"
Nikamjibu " Yah Angel ndo nimeiona sasa hivi nashuka Ubungo hapa nikawa nataka nikupigie"

"Ooooh thanks God! Yaan you can keep hizo hela but please naomba nihifadhie vitambulisho vyangu ni muhimu mno yani"
"Whaaat?? Hela zote hizi? Are you serious?"

"Yah, why not? Cha msingi naomba nitunzie tu vitambulisho ntavifuta vyote.."
"Sawa, usiku mwema Angel, ahsantee"
"Usijali.. Usiku mwema pia"

Dah, ni kama nilichanganyikiwa ghafla.. Zile pesa hazipungui kama Milioni 5 hivi... Yaani zangu zote Nikaona ni zali la mentali.

Nikawa nawaza, sijui nikodishe Taxi? Au nilale Blue Pearl hadi kesho? Wakati nawaza hayo, mara nasikia..

"We Kidevu Umejilaza tu hapo kwenye mkeka maharage hata huangalii, hivi umeongeza mkaa kweli? Na yakiungua hayo utakula ugali na
chumvi..."

Dah, mama yangu kaniamsha nilikuwa ndotoni, tena usingizi wa mchana..Duuh!!!
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: