SHIRIKA linalotetea haki za watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) la Under The Same Sun (UTSS), limelaani vikali mauaji ya kikatili yaliyotokea mkoani Simiyu.

Mauaji hayo yaliyotokea Jumatatu ya wiki hii katika kijiji cha Mwachalala, Wilaya ya Bariadi mkoani humo, yamesababisha kifo cha Munghu Lugata (40), ambaye alikutwa amekufa nje ya nyumba yake na mwili wake umenyofolewa mguu, vidole viwili vya mkono wa kushoto na kidole gumba.

Akitoa tamko mbele ya vyombo vya habari, Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo, Vicky Ntetema alisema, bado maalbino wamekuwa wakiishi kwa hofu ndani ya nchi yao wenyewe kutokana na mauaji hayo kuendelea.

“Tunatoa tamko la kulaani vikali mauaji ya watu wenye albinism, ukatili kwa watu wenye albinism, mauaji haya yamekuwa yakiendelea na kuwapa hofu,” alisema Vicky.

Alisema kwa mujibu wa taarifa walizonazo Munghu anakuwa ni mtu wa 73 kuuawa na watu ambao wana fikra potofu juu ya watu hao. Alisema walipata taarifa kutoka kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Charles Mkumbo kuwa mwanamke huyo aliuawa usiku wa kuamkia Mei 12, mwaka huu.

“Alidokeza kwamba siku moja kabla ya kifo chake ambaye ni mama wa watoto wawili alimtuma mtoto wake mmoja ambaye siyo albino akamchukulie dawa kwa mganga wa kienyeji kwa kuwa alikuwa akiumwa.

“Gudawa ambaye ndiye mganga wa kienyeji alimwambia mtoto huyo dawa hiyo aifuate kesho na la ziada alimtaka mtoto huyo asirudi nyumbani kwa mama yake anayeugua kwa madai kwamba dawa itafanya kazi vizuri ikiwa atalala mbali na mama yake,” alisema.

Alisema kwa mujibu wa Kamanda Mkumbo tayari watu wawili wanashikiliwa ambapo watu hao mama Gudawa Yalema (52) na Shiwa Masalu (45).

Alisema waganga wa kienyeji wamekuwa wakiwarubuni wateja wao kuwa ngozi, nywele, damu na viungo vingine vikichanganywa na uchawi vinawahakikishia mafanikio na utajiri.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: