Msanii wa filamu za maigizo nchini kutoka kambi ya Bongo Muvi, aliyejizolea umaarufu miaka ya hivi karibuni, Adam Kuambiana aliyeaga dunia juzi Jumamosi, anatarajiwa kuzikwa kesho Jumanne kwenye makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam alipozikwa msanii mwenzake, Steven Kanumba.

Akizungumza na vyombo vya habari, Rais wa Bongo Muvi, Steve Mengere ‘Steve Nyerere’, alisema ratiba iliyopo ni leo asubuhi waombolezaji wameuchukua mwili  wa marehemu hospitali ya Taifa ya Muhimbili na wameupeleka nyumbani kwake Bunju B jijini Dar na Jumanne watauchukua mwili wa marehemu na kuupeleka Viwanja vya Leaders Club kwa ajili ya mazishi ambayo yatafanyika katika makaburi ya Kinondoni jijini.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: