Meneja wa Huduma kwa jamii wa Airtel Bi Hawa Bayumi (Kulia) akikabithi msaada wa vifaa vya ofisi ya walimu kwa mwalimu mkuu wa shule ya msingi Buyuni Bwana Amiri Mkojela wakati Airtel ilipotembealea shuleni hapo na kutoa viti na meza kwa ajili ya ofisi ya walimu , wakishuhudia katikati ni Mwenyekiti wa Shule, Jamhuri Masiku, na wanafuanzi wa shuleni hapo, hafla ya makabidhiano ilifanyika shuleni hapo mwishoni mwa wiki hii.
---
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.

kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imetoa msaada wa seti ya meza na viti vya ofisi za walimu katika shule ya msingi Buyuni iliyopo Kata ya Pembamnazi, Manispaa ya Temeke Jijini Dar es salaam.

Msaada wa vifaa vya ofisi wenye thamani ya shilingi million tatu na nusu umetolewa kwa ajili ya walimu kufatia uhaba wa viti vya kukalia pamoja na Meza shuleni hapo.

Akizungumza wakati wa kukabithi vifaa hivyo Meneja wa Huduma kwa jamii wa Airtel Bi Hawa Bayumi alisema” Airtel tumejikita katika kusaidia sekta ya elimu kupitia mradi wetu wa Shule yetu kwa kutoa msaada wa vitabu mashuleni, lakini leo tumeamua kuwaangalia walimu na kuwawezesha kuwa na mazingira mazuri zaidi ya kufanyia kazi na kuwapatia viti na meza kwaaji ya ofisi zao kwani tunatambua kuwa walimu wanamchango mkubwa sana kwa wanafunzi na jamii kwa ujumla”

“Tunaamini mchango huu utaleta ufanisi katika kazi zao na kuongeza ufanisi zaidi,
“Airtel tumejipanga kuendelea kujikita katika kusaidia elimu kwa kuwawezesha walimu pamoja na wanafunzi kupata nyenzo muhimu katika elimu ili kuleta chachu ya maendeleo ya elimu nchini na ufaulu wa wanafunzi katika masomo yao” aliongeza Bayumi

Akiongea mara baada ya kupokea msaada huo Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Buyuni Amiri Mkojela alisema” Msaada huu umekuja kwa wakati muafaka ambapo shule yetu ina upungufu wa vifaa vya ofisi ya walimu. meza na viti hivi tulivyopokea leo vitaboresha mazingira ya ofisi zetu kuwa ya kisasa zaidi na kuwawezesha walimu wetu kusahihisha kazi na mitihani ya wanafunzi na kuaandaa vipindi vyao katika mazingira yaliyo bora zaidi. Tunawashukuru sana Airtel kwa kutufikishia msaada huu leo shuleni hapa na tunaomba waendelea na juhudi hizi kwani zina mchango mkubwa katika jamii.

Kampuni ya Airtel imekuwa ikitoa misaada kwa jamii hususani katika sekta ya elimu , chini ya mpango wake wa Airtel Shule yetu zaidi ya shule 900 za sekondari zimeweza kufaidika na msaada wa vitabu vya ada na kiada na kupunguza tatizo la uhaba wa vitabu kwenye shule hizo
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: