KWELI TUMEFIKA HAPA - Wanafunzi wa St. Augustine wamemuua mwenzao Herman Michael 22 kwa kumkuta na laptop zilizoibiwa toka kwa baadhi ya wanafunzi wa chuo hicho. 

Huu ndiyo usomi wa siku hizi? hii ndo elimu tunayopewa sasa? Ndo viongozi hawa tunaowatarajia?? Sasa kama wasomi tunafanya hizi je mtaani vitendo hivi vitakwisha????? 

1. Ilitosha tu kumpeleka polisi kwa udhibitisho wa laptop zilizoshikwa 

2. Kazi ya Dean of Students chuoni hapo ni nini? kwanini huyu kijana hakupelekwa kwa Dean? 

3. Undugu na umoja wa wanafunzi wa St. Augustine upo kweli? (Sijasoma hapo ila nina amini wanafunzi wa chuo kimoja ni wamoja) unawezaje kunyanyua jiwe na kumrushia mwenzako wa zizi moja? 

4. Nakiheshimu chuo kile sana ila kweli elimu itolewayo pale inaweza kuruhusu MAUAJI yafanyike na WASOMI watarajiwa wa palepale???? 

5. Je mliofanya hayo mauaji mnadhani mmekiweka chuo wapi katika muonekano wa ajira? na muonekano wa kijamii? # R.I.P kijana uliyeuwawa, Vyuo tuajiri PSYCHOLOGISTS ambao watawasaidia vijana wenye abnormal behavior kama za Marehemu husika pamoja na wanafunzi wauaji#

Maoni haya yametolewa na  Cannon Luvinga.

Kama na wewe unakero/maoni yako yanayokugusa toka pande zozote za dunia, usisite kuwasiliana nasi kwa anwani; cathbert39@gmail.com/0787999774

MWANAFUNZI WA CHUO KIKUU CHA SAUT JIJINI MWANZA AUAWA NA WANAFUNZI WENZAKE KWA TUHUMA ZA WIZI.

Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino (SAUT) cha jijini Mwanza, Helma Michael (22) ameuawa kwa kupigwa mawe na wanafunzi wenzake, wakimhisi kuwa ni mwizi wa kompyuta ndogo za mkononi na deki chuoni hapo.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Valentino Mlowola, alisema juzi kuwa mwanafunzi huyo aliuawa Mei 13 mwaka huu saa 4.00 usiku, katika eneo la Nyamalango Malimbe, ambapo baada ya kubainika katika eneo hilo alianza kupigwa kwa mawe, fimbo na mapanga hadi kusababisha kifo chake: “Huyu ameuawa katika tuhuma ambazo mpaka sasa hazijathibitishwa,” alisema.

Kutokana na mauaji hayo, watu 17 wamekamatwa na Polisi imeanza uchunguzi kuhusu tukio hilo huku Kamanda Mlowola akiwataka watu kutojichukulia sheria mkononi kwa kuwaua watu ambao hawana hatia.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: