Na Mohammed Mhina, Handeni.

WILAYA ya Handeni mkoani Tanga imetangaza kuwa haitaomba tena chakula cha mtaada kutoka serikali kuu kwa msimu ujao kutokana na matarajio ya kuvuna kiasi kingi cha mazao yakiwemo mahindi na ufuta ikilinganishwa na miaka mingine iliyopita.

Mkuu wa wilaya ya Hendeni mkoani Tanga Bw. Muhingo Rweyemamu alitoa kauli hiyo wakati wa ziara yake ya kuwatembelea wakulima katika vijiji mbalimbali vya wilaya hiyo kuangalia utekelezaji wa maagizo ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya hiyo ya kumtaka kila mwananchi kulima kwa bidii na kupanda kwa kufuata maelekezo ya wataalam.

Akiwa katika mashamba ya wakulima wa vijiji vya Manga, Kwamsisi, Kang’anta, Madebe, Misima, Sindeni, Mzeri na Mbagwi wilatyani Handeni, Mkuu huyo wa wilaya Bw. Rweyemamu alisema katika msimu ijao, wilaya hiyo haitaomba tena chakula cha msaada kwa vile wana uhakika wa kuvuna chakula cha kutosha.

Amesema pamoja na kwamba mvua zinazoendelea kunyesha nchini kote zimekuwa zikileta madhara kwa baadhi ya maeneo, lakini kwa wilaya ya Handeni mvua hizo zimeleta neema na faraja kwa wakulima kutokana na kuimarika kwa mazao yao mashambani.

Bw. Rweyemamu amesema karibu ya maeneo mengi wilayani humo, wamepata mavuno ya kutosha hasa mahindi na ufuta.

Naye Afisa Kilimo wa Wilaya ya Handeni mkoani Tanga Bw. Yibarik Chiza, amesema kuwa wakulima wengi katika wilaya hiyo wamelima kwa kutumia trekta na majembe ya kukokotwa kwa wanyamakazi jambo ambalo amesema litawaongezea ufanisi mkubwa msimu huu.

Na kwa upande wao baadhi ya wakulima wilayani humo wamesema chakula kitakachopatikana msimu huu wilayani humo hakijawahi kupatikana zaidi ya miaka 30 iliyopita
 Mmoja ya wakulima wa Mahindi Wilaya ya Handeni mkoani Tanga Bw. Adalbertus Bubelwa wa pili kutoka kushoto akimwelezea Mkuu wa wilaya ya handeni Bw. Muhingo Rweyemamu, jinsi alivyoandaa shamba lake. Mkuu huyo wa wilaya alikuwa katika ziara ya kuwatembelea wakulima katika vijiji mbalimbali wilayani humo kuangalia mazao mashambani.
 Mkuu wa wilaya ya Handeni Bw. Muhingo Rweyemamu, kushoto ambaye ni mwenye shamba akipata maelekezo kutoka kwa Afisa Kilimo wa Wilaya hiyo Bw. Yibarik Chiza, aliyemtembelea Mkuu huyo wa wilaya shambani kwake.
 Sehemu ya mashamba ya mahindi katika maeneo mbalimbali wilayani Handeni.
Shamba la mahindi katika kijiji cha Manga likionekana kustawi vya kutosha.

 Mkuu wa wilaya ya Handeni Muhingo Rweyemamu (kushoto) akisalimiana na mmoja wa walimu shuleni hapo wakati wa ziara yake.
 Mkuu wa wilaya ya Handeni Muhingo Rweyemamu (wapili kushoto) akitoa maelekezo kwa walimu wa shule ya sekondari Magamba.
Mmoja wa Wakulima wa Ufuta katika Kijiji cha Misima wilayani Handeni Bw. Rashidi Dempombe, akimweleza afisa Kilimo wa wilaya hiyo Bw. Yibarik Chiza, kwa namna alivyolima na kupanda zao hilo ambalo ni la biashara.
Afisa Kilimo wa wilaya ya Handeni mkoani Tanga Bw. Yibarik Chiza, akiwaelekeza jambo wakulima wa zao la ufuta wa Kijiji cha Misima wilayani humo
  Ufugaji wa kuku wa kisasa katika wilaya ya Handeni mkoani Tanga ni moja ya shughuli zinazowapatia wananchi fedha za ziada.
 Mmoja ya wakulima wakubwa wilayani Handeni Bw. Rory Nighngale, katikati akimwelezea Mkuu wa wilaya ya Handeni Mkoani Tanga Bw. Muhingo Rweyemamu kulia alipotembelea katika shamba hilo akiongozana na Afisa Kilimo wa wilaya ya Handeni Bw. Yibarik Chiza kuona ana ya mananasi katika shama hilo lililopo katika eneo la Kwamsisi wilayani humo.
 Mmoja wa wakulima wa nanasi wilayani Handeni Bi Sabrina Rory Sasumua, akionyesha aina ya nanasi lenye uzito wa kilo mbini na nusu kutoka katika shambani lake eneo la Kwamsisi wilayani Handeni.
 Mkuu wa wialya ya Handeni Muhingo Rweyemamu akihudumia mifugo yake baada ya saa za kazi.
 Mkuu wa wialya ya Handeni Bw. Muhingo Rweyemamu, kulia akipokea fimbo mbili zilizotengenezwa kwa mpingo kutokaka kwa Mzee Adam Hassan Mtii wa Kijiji cha Mbagwi kilichopo kata ya Misima wilayani humo. Mzee Mtili ameagiza moja ya fimbo hizo apelekewe Rais wa Jamhuri ya Muungano Dk. Jakaya Kikwete.
 Mkuu wa wilaya ya handeni Bw. Muhingo Rweyemamu, akisalimiana na mmoja wa wananchi alipotembelea katika kijiji cha Kang'anta kuangalia maendeleo ya mdada wa mifugo na mazao ya chakula na biashara.
Baadhi ya akina mama wa eneo la Sokoni katika wilaya ya Lushoto mkoani Tanga wakifanya biashara za matunda na mbogamboga. (Picha Zote na Mohammed Mhina).
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: