SHILINGI INA PANDE 2, kamwe Usiamini Ukweli wa Upande 1 tu wa Shilingi Mara nyingi unapoanza Uhusiano mpya na mtu kuna tendency ya kuuliza-uliza maswali ya kibwege-bwege tu madai yake anapeleleza PAST ili ajue pa kuanzia...PAST sio Mtaji wa FUTURE, Mtaji wa FUTURE ni STATUS QUO (Present)

Ukimjudge Cosmas Chidumule wa leo kwa vitu alivyofanya akiwa na bendi ya DDC MLIMANI PARK ORCHESTRA mwaka 1979 utafeli kwa sababu leo hii ni Mwimbaji wa Injili mwenye Good Present.
UTASIKIA, ''Demu wako mlidumu Miaka Mingapi, sasa kwanini Mliachana???, Nani alikuwa mkorofi kati yenu??? ''Hivi unategemea mimi ntajibu nini kama sio Kupaka rangi chuma changu chenye Kutu na kusema EX wangu ndiyo mwenye makosa hata kama ni mimi nilisababisha tuachane??? Lazima nijifagilie, I was so inlove ila nikaumizwa, please don't hurt me again, nitatoa na vichozi kama robo lita hivi, basi unaingia kingi... UMELIWA.

Ukiingia Penzini na Mtu PUNGUZA MASWALI YA KIKUKU, Msikilize ANA NINI SASA, Je anakupenda na anawaza nini kuhusu FUTURE yenu, Full Stop, ukianza kujifanya TAKUKURU kuchunguza Dhambi za Jambazi aliyetubu na Changudoa anayeimba Kwaya ni aidha utadanganywa tu au utaumia moyo wako bure.

UKIMCHUNGUZA SANA BATA HUTAWEZA KUMLA... Punguza u-TAKUKURU wa Mahaba maana Kuna watu wana PAST chafu kuliko Boxer ya Kichaa akiamua kufunguka utajikuta unanena kwa lugha ohhh rikabababababantashakaratarobosiKANTANGAZEyashikabasethkatisharogeroshantahaymah.

Imetolewa na Seth Giovanni.
Mkuu wa Chuo cha Mapenzi.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: