Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.

MKALI wa muziki wa kizazi kipya, Mbwana Mohamed Mb Dog, amesifia video ya wimbo wake mpya ya Mbona Umenuna akisema imeandaliwa kwa kiwango cha juu na kudhihirisha ubora wake.

Akizungumza leo asubuhi jijini Dar es Salaam, Mb Dog alisema mashabiki wote watakaopata bahati ya kuitazama video hii iliyotengenezwa na Abby Kazi, ataamini makali yake.

Alisema lengo lake ni kuwapatia mashabiki burudani kamili, hivyo wadau wote wapate muda wa kuitazama video hiyo iliyoachiwa rasmi mwishoni mwa wiki iliyopita, sambamba na kuingizwa kwenye mitandao ya kijamii, youtube na blogs.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: