Mshiriki akiimba mbele ya majaji katika shindano la Epiq Bongo Star Search (EBSS) jana ambapo washiriki watano walitolewa.
Jaji Mkuu wa shindano la Epiq Bongo Star Search (EBSS) Ritha Paulsen akimwelekeza jambo mmoja kati ya washiriki wa shindano hilo.
Mshiriki mwanadada akifanya manjonjo yake wakati wa shindano hilo lililooneshwa jana.
Mshiriki akipita mbele ya wenzake baada ya kutolewa katika shindano hilo

Mshiriki akipita mbele ya wenzake baada ya kutolewa
Mtangazaji wa kipindi hicho Siza Daniel akiwa mbele ya washiriki ambao walikuwa wameingia katika danger zone
---
• Namba za kuwapigia kura washiriki kutolewa wiki ijayo
• Washiriki 10 wamebaki mpaka sasa

Washiriki wawili ambao wamefanikiwa kuingia kwenye fainali za shindano la kuimba la Epiq BSS kwa njia ya simu watajulikana jumapili hii, baada ya kuwashinda wenzao zaidi ya elfu 3000 walioshiriki shindano hilo kupitia simu ya mkononi.

Washiriki hao wawili wataungana na wenzao kumi, ambao jana walifanikiwa kuingia hatua hiyo kati ya kumi na tano waliokuwa wamebaki.

Mashabiki wengi wa shindano hilo wanawasubiria kwa hamu washiriki hao hasa baada ya mshiriki kwa njia ya simu wa mwaka jana, Menina Atick, kufanya vizuri.

Mpaka sasa wamebaki washiriki kumi ambao ni Amina Chibaba, Elizabeth Mwakijambile, Emmanuel Msuya, First Godfrey, Francis Flavian, Furaha Charles, Furaha Mkwama, Joshua Kahoza, Maina Thadei na Mandela Nicolus.

Washiriki walioga jana ni Fatma Omary mshiriki kutokea Dar es salaam, Joseph Kura mshiriki kutokea Arusha na Catherine Mtange akitokea Dar es salaam.

Wengine walioaga ni pamoja na Joseph Meteka na Kenedy Gedeon ambapo washiriki ambao walitolewa kwenye danger zone na kurudia katika kundi la washiriki wa kawaida ni Furaha Mkwama na Mandela Nikolas.

Shindano hilo ambalo limeanza kushika kasi sasa, linanogeshwa na meza ya kitivo, ambayo inasaidiana na majaji.

Wiki hii meza ya kitivo ilikuwa na mtayarishaji wa muziki, Lamar, pamoja na mwanamuziki Rich Mavoko.

Akizungumzia hatua ambayo shindano limefikia, jaji mkuu wa shidano hilo, Ritha Paulsen, alisema kuanzia wiki ijayo watawapa nafasi wananchi waanze kuwapigia kura washiriki wanaowapenda.

‘Hatua hii ni muhimu sana, hasa kwa kuwa inarirudisha shindano kwa wananchi ili waweze kumchagua mshindi wao’ alisema Ritha.

Akizungumzia ubora wa washiriki wa mwaka huu, Ritha alisema wamepata washiriki bora zaidi, na pia mafunzo wanayoyapata ndani ya jumba la Epiq BSS ni makubwa hivyo mashabiki watarajie mchuano mkubwa zaidi katika kuwania milioni hamsini.

Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: