edd’s Miss Tz Hapiness Watimanywa katikati akizungumza na waandishi wa habari kwenye ofisi za Kampuni ya bia nchini TBL juu ya ushindi wake wa Taji la Miss Tz 2013 kulia ni Mkugenzi mkuu wa Tbl Nchini Robin goestzche na kushoto ni Mkugenzi wa masoko wa TBL Kushila Thomas.

  Meneja masoko wa TBL Fimbo Buttala akijibu moja ya maswali ya waandishi wa habari kwenye tafrija fupi ya kumtambulisha Redd’s Miss Tz kwa mkurugenzi mkuu wa Tbl Robin goestzche
 Mkurugenzi mkuu wa Tbl nchini Tanzania Bwana Robin goestzche akimpongeza Redd’s Miss Tz 2013 Hapiness Watimanywa na kushoto ni Mkugenzi wa masoko wa TBL Kushila Thomas.
 Redd’s Miss Tz Hapiness Watimanywa katikati akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi mkuu wa Tbl Robin goestzche na kushoto ni Mkugenzi wa masoko wa TBL Kushila Thomas katikati yao ni kushoto kwake ni mshindi wa shindano la Redd’s Miss Tz Latifa Mohamed na mshindi wa tatu Clara bayo.
 Redd’s Miss Tz Hapiness Watimanywa katikati akiwa katika picha ya pamoja viongozi mbalimbali wa kampuni ya bia nchini Tbl.
Meneja masoko wa Tbl Nchini Fimbo Buttal akimpongeza mshindi wa shindano la Redd’s miss Tz 2013 Hapiness Watimanywa mara baada ya kukamilisha mazungumzo ya utambulisho kwa Mkurugenzi mkuu wa Tbl nchini Tanzania.
---
Na Mwandishi Wetu

REDD’S Miss Tanzania, Happiness Watimanywa jana alitembelea rasmi Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) walio wadhamini wa shindano hilo, ambapo alikutana na uongozi wa juu ili kujitambulisha.

Katika ziara hiyo, Happiness alifuatana na mshindi wa pili, Latifa Mohammed, mshindi wa tatu, Clara Bayo pamoja na Kamati ya Redd’s Miss Tanzania.

Akizungumza mara baada ya kukutana na mrembo huyo, Mkurugenzi Mkuu wa TBL, Robin Goestache alisema, wao kama wadhamini wakuu wanajisifu kuwa sehemu ya mafanikio ya Redd’s Miss Tanzania, huku akimsifu mrembo huyo kwa ushindi wake.

“Kila mmoja kati yetu anajua shindano lilivyokuwa gumu, warembo wote walikuwa na sifa na ninawapongeza ninyi mlioshinda na tunawakaribisha katika familia ya TBL,” alisema.

Mkurugenzi wa Masoko wa TBL, Kushillah Thomas, naye alitumia fursa hiyo kuwapongeza warembo hao na kusema ana imani kubwa nao watafanya vizuri zaidi katika kipindi chao.

Meneja Masoko wa TBL, Fimbo Butallah alisema, toka waanze kudhamini shindano hilo wamepata mafanikio makubwa mno, huku kukiwa na kazi nyingi za jamii wanazozifanya na warembo waliofanikiwa kutwaa taji hilo.

Happiness naye aliishukuru TBL kwa kudhamini shindano hilo na kusema anajivunia kwa kiasi kikubwa kuwa sehemu ya familia ya Redd’s.

“Kwa kiasi kikubwa nawashukuru kutokana na kudhamini shindano hili kwa muda wa miaka 13, kwani mmesaidia mengi kwa warembo na najivunia kuvaa sura ya Redd’s.”

Shindano la Redd’s Miss Tanzania kwa sasa linadhaminiwa na kinywaji cha Redd’s Original kinachozalishwa na kusambazwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: