Jambo moja kubwa ambalo jamii imekuwa ikilikemea mara kwa mara ni suala la wizi, wizi umekuwa ukirudisha maendeleo ya wanajamii sehemu yeyote.

Kisa kilichonikuta jumapili ni pale nilipotoka nyumbani majira ya saa 2:07 asubuhi naelekea kanisani (St. Peters) mbuyuni jijini Dar na baada ya kufika nilipaki gari eneo la kanisa la St. Peters na kuingia kanisani kusali. Muda ulipofika wa kutoka, tulitoka na kuelekea kwenye gari langu. Niliingia kwenye gari na kuwasha kisha nikaondoka eneo la kanisa, mita chache kabla sijavuta mataa ndipo niliposikia gari langu linamlio tofauti wa taa za indicator (taa za alama za kushoto ama kulia). 

Ilinibidi nivuke eneo hilo na baadae nisimame mbele kabisa na kushuka kuangalia nikakuta wameiba taa za gari, taa za mbele (Conner lamp). Sikuweza kushtuka hapo hapo bali baada ya kuondoka. Ukiangalia eneo hilo wapo walinzi wa kutosha kabisa.

Kiukweli kitendo kile kilinisononesha sana na kurudi eneo la tukio na kuwaita walinzi na kuwaambia kuwa nimeibiwa wao wakaanza kunipa pole ambayo kiukweli haikunisaidia lolote.
Baadae niliona wanaanza kubishana wenyewe, unajua nilishawaambia hawa viongozi haya mambo ya kuvaa hivi vinguo (nguo za alama za kuwaonyesha kuwa ni walinzi) siyo vizuri maana wale wezi wanatuvizia tunaangalia magari upande wa kule (kulia) na huku (kushoto) wanaiba.

Mimi niliwauliza kitu kimoja tu, inakuwaje mnaibiwa wakati na nyie mpo? akanijibu "Unajua tena kaka haya mambo ya wizi wala hayapingiki ila tambua hawa wezi wanaiba hasa wakituona tumeenda kuangalia usalama wa magari ng'ambo,".

Sikufurahiswa sana na majibu ya wale walinzi nilichokifanya niliwaaga vizuri na kuwaambia wawe makini na magari ya watu, nikaingia kwenye gari na kumshukuru Mungu kwa lililotokea.

Kikubwa ninachowaambia ndugu zangu mnaoenda kusali kanisa la St. Peters eneo lile si salama bado ule wizi wa kipindi cha nyuma unaendelea wala hakuna haja ya kuficha ni vyema tuliseme ili watu waendelee kuwa makini. Na viongozi waweze kuimarisha ulinzi.

Asanteni sana ni mimi yaliyonikuta Cathbert Angelo mmiliki wa Kajunason Blog.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: