Dun and Bradstreet Credit Bureau Tanzania Limited, Ofisi ya kwanza yenye kibali cha kutunza kumbukumbu za Mikopo Tanzania, imepanga kukutana na kushauriana na watendaji wakuu wa Benki zote Tanzania katika semina itakayofanyika Jijini Dar es Salaam katika Hotel ya Hyatt-Kilimanjaro siku ya tarehe 3/05/2013.
Warsha hiyo itaambatana na utambulisho na ufunguzi wa ofisi ya Dun and Bradstreet Credit Bureau Tanzania Limited nchini Tanzania, semina hii inalenga kukuza mahusiano kati ya ofisi hii, mabenki na taasisi zote za kifedha ambazo zimeleta mchango muhimu katika kuhakikisha kwamba wanapata ofisi ya kudhibiti kumbukumbu za mikopo yenye viwango vya kimataifa.
Kwa mujibu wa Bw. Miguel Llenas – Mkurugenzi Mkuu wa Dun & Bradstreet Credit Bureaus Limited “ Lengo kuu ni kujenga taasisi itakayoweza kusimamia jukumu la kuinua uchumi wa Tanzania na utimamu katika taasisi za fedha na Benki.
Kwa maana hii, semina itaeleza kwa kina jinsi ya kusaidia benki na taasisi za fedha nchini Tanzania juu ya kutathimini na kuboresha maombi ya mikopo/mkopo kwa lengo la kuhakikisha kwamba wanakuwa na habari na utambuzi juu ya waombaji wa mikopo katika mabenki na taasisi zao.
Pia, katika warsha/semina hii, meneja mkuu wa Dun & Bradstreet Credit Bureau Tanzania Limited - Adebowale Atobatele amesema “Tumeangazia mabenki na taasisi za fedha nchini Tanzania kuwa washirika wetu. Fursa pekee ya kukutana, kusikilizana na kushauriana na washirika wetu katika hili ni semina. Tunahitaji kuwatumikia wao na ni muhimu kuelewa changamoto husika wanazokumbana nazo katika biashara hii ya ukopeshaji. Tunaamini ufumbuzi wa kuendeleza maslahi bora ya mabenki, sekta za fedha na uchumi watanzania, na watanzania kiujumla ni kwa kupata michango mbalimbali kutoka katika benki na taasisi za fedha ambazo zitakutanisha taarifa za mikopo zitakazotambuliwa katika kiwango cha kimataifa”.
Kwa muda mrefu, mabenki na taasisi za fedha nchini Tanzania zimekuwa zikiweka kumbukumbu juu ya uwiano wa mikopo isiyofanya vizuri katika vitabu vyao kiasi inafikia kiwango cha kusamehe madeni hayo na kurekodi faida ndogo. Uanzilishi wa taasisi ya kutunza kumbukumbu za mikopo katika mifumo ya kibenki, taasisi za kifedha na wateja, itasaidia kuleta mwangaza katika siku zijazo.
Semina ya tarehe 3 mwezi wa 5 itakayoandaliwa na Dun and Bradstreet inafuatiwa na mafanikio ya shughuli zake katika ofisi zilizopo Ghana ambapo soko lake limekuwa kubwa kwa uwepo wa D&B
Uwepo wa Dun and Bradstreet Credit Bureau nchini Tanzania unategemewa kwa kiwango kikubwa kuimarisha na kujenga daraja kati ya Benki ya Tanzania na Sekta za Benki.
Toa Maoni Yako:
0 comments: