WAREMBO wenye sifa za kushiriki shindano la Redds Miss Tanga 2013, wametakiwa kujitokeza kushiriki shindano katika kuwania taji la Miss.

Akizungumza na Vyombo vya Habari Mkurugezi wa Kampuni ya DATK Intertaimeint, Asha Kigundula alisema kwa maandalizi ya shindano hilo ndiyo yanaanza na kutaka warembo wajitokeza kushiriki.

Asha alisema fomu zitapatikana katika ofisi ya Mwananchi iliyopo bandari Tanga gorofa ya Nne, Five brothers kwa Nassa Makau iliyopo jijini humo, kwa Dar es Salaam zinapatikana katika ofisi za Jambo Leo zilizopo jingo la Hifadhi Hause Posta.

“Mazoezi kwa warembo yataanza ijumaa ya Mei 3 mwaka huu jijini Tanga, warembo hao watakuwa chini ya walimu wawili ikiwa ni pamoja na mshindi wa mwaka jana wa mkoa huo Teresia Kimolo”alisema Asha.

Alisema kwamba shindano la mwaka huu litaandika historia mpya ya urembo mkoani humo kwa kuwa Kampuni DATK imejipanga, hivyo mashabiki wa mashindano ya urembo wa jijini hapo kwa ujumla wakae mkao wa kupata raha.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: