Zaidi ya waumini 5,000 wa zehebu la Kikristo hapa nchini na nje ya nchi, wanatarajia kuudhulia mkesha wa AFLEWO unaotarajia kufanyika leo katika Ukumbi wa Kanisa la BCIC Mbezi jijini Dar es Salaam.
Mkesha wa AFLEWO kwa kirefu ‘Africa Let’s Worship’ kwa hapa nchini ulianzishwa 2011, ambapo ulikufanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee na kushirikisha watu kutoka nchi za jirani Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na Nigeria.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Askofu Fredy Kyara Cpichani katikati) alisema, mkesha huo utaanza saa 3:00 usiku mpaka majogoo huku akidai kuwa, kwa waumini watakaojitokeza kwenda kutakuwa na mabasi Mwenge katika sheli ya Puma kwa ajili ya usafiri mpaka kanisani hapo.
“Mkesha huu, ambao hauna kiingilio, una lengo la kuomba, kuabudu na kusifu, hivyo basi wanaomba watu wajitokeze kwa wingi kuja kujumuika nasi katika mkesha huo,”alisema Kyara.
Aidha Kyara alisema, wahusika katika mkesha huo ni waumini na waimbaji kutoka katika makanisa mbalimbali na kudai kuwa kutokana na maana ya AFLEWO, kutakuwepo na wawakilishi kutoka Kenya, Rwanda na nchi nyingine za Afrika.
Alisema, lengo kubwa la kuufanya mkesha huo kutokuwa na kiingilio ni kwa sababu sio tamasha, hivyo basi hawana budi kuufanya bure ili kila mtu awe na nafasi ya kumwabudu mungu na kuliombea Taifa kwa ujumla.
Aliongeza kuwa, kutokana na nia ya AFLEWO, Julai mwaka huu wanatarajia kufanya mkesha jijini Mwanza na baadae Jijini Arusha, na kudai kuwa kwa Tanzania ni mwaka wa tatu sasa, kwa kuwa mkesha huu ulianzia Kenya, Rwanda, Burundi, Nigeria na sasa Tanzania.
Toa Maoni Yako:
0 comments: