Tigo Tanzania wamezindua ukurasa wake mpya wa Twitter wa kuchati moja kwa moja , huduma ya kipekee na ya kwanza Tanzania , ambapo wapenzi wa Tigo Twitter wanaweza kuchati na mastaa wawapendao moja kwa moja kwa njia ya mtandao huo kwa muda wa saa nzima. Kwa kuanzia, mashabiki wa msanii maarufu wa Tanzania, Elias Barnaba, wamepewa fursa ya kuchati moja kwa moja na msanii huyo ikiwa ni pamoja na kumuuliza maswali ambapo atayajibu papo hapo.
Meneja Chapa wa Tigo Bw William Mpinga alisema wakati wa uzinduzi kuwa, “Tigo inajivunia kuwapa wapenzi wa Tigo Twitter jukwaa la kuonana na kuchati moja kwa moja na mastaa wawapendao kupitia ‘Twitter Celeb Live Chat’, ambapo wataweza kufurahia na kubadilishiana nao uzoefu wa maisha yao kwa ujumla; huduma maalumu ya kipekee kabisa na ya kwanza Tanzania kutoka Tigo! Kupitia Jukwaa hilo maalumu , Staa maarufu wa muziki wa kizazi kipya Barnaba ambaye ndiye staa wa kwanza kushriki katika jukwaa hilo, atapokea maswali moja kwa moja kutoka kwa mashabiki wake na kutoa majibu papo kwa papo, jambo ambalo mashabiki hawakuwahi kulifikiria kabla..”
"Ningependa kuwaarifu wateja wetu wote na wale wapenzi wetu wa Tigo Twitter kuwa hii ni mojawapo ya huduma bora kabisa za burudani za kuchati moja kwa moja ambapo nyingine nyingi za aina hii ziko njiani! Hii ni fursa ya pekee ya kufurahia maisha na ninatoa wito kwa wote kuijunga na mtandao wa Tigo Twitter na kuungana nasi ili kufuarahia mambo mazuri yanayofanywa na kuwezeshwa na mtandao wa Tigo. “ alifafanua zaidi Bw. Mpinga.
Hivi karibuni, Tigo Tanzania ilipata tuzo ya utambuzi ya dunia kwa kuwa kampuni pekee inayowasilaina na wateja wao moja kwa moja kupitia kurasa za mtandao mbalimbali ya kijamii kama Facebook. Hii ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na shirika la SocialBakers mnamo tarehe 7, Februari 2013, ikijumuisha chapa kumi bora za kijamii duniani kwenye mtandao wa wa Facebook katika robo ya mwisho wa mwaka 2012. Huduma ya kuchati moja kwa moja na mastaa mbalimbali ni njia ya kipekee ya Tigo kuwaunganisha, na kuwafanya wateja wetu wapendwa kujumuika kwa pamoja kupitia majukwaa mbalimbali ya habari ya kijamii ambayo wanayapenda.
Kushiriki katika huduma hii ya kuchati moja kwa moja unahitaji kuungana na Tigo Tanzania kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter, kisha tumia #OngeanaTigoCeleb na weka Tigo using @Tigo_Tz @jina la celeb
Kama haujaiunga na mtandao wa Twitter, tafadhali tumia hatua rahisi zifuatazo ili kuweza kunufaika huduma hii bomba ya Tigo:
Andika @Tigo_Tz kwenye search kisha bofya
Utatokea ukurasa wa Tigo. Bonyeza kwenye follow.
Baada ya hapo rudi kwenye ukurasa wako wa Twitter na utaweza kuziona Tweet za Tigo na celeb
Toa Maoni Yako:
0 comments: