Na Kajunason Blog team, Dar es Salaam

Watu zaidi ya 10 wamenusurika kifo kutokana na kipigo cha wananchi, kwa kile kilichodaiwa kutumwa na mfanyabiashara wa vipodozi, S.H Amon, kuvunja nyumba ya mkazi wa Sinza E, Aristedes Ishibabi.

Sakata la watu hao ambao ni mabaunsa, lilitokea Dar es Salaam, ambapo watu hao walioongozwa na mmoja wa mabaunsa hao aliyetambulika kwa jina moja la Joseph, inadaiwa walikuwa na madalali tumwa na Kampuni ya udalali ya Majembe Auction Mart.

Akizungumzia tukio hilo, Mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Sinza E, Robert Ngoti, alisema watu hao walivamia nyumba hiyo saa 11 alfajiri na kutaka kumtoa mke wa mwenye nyumba hiyo, Anitha Aristedes, lakini kutokana na ushirikiano wa wananchi watu hao walijikuta wanagonga mwamba.

“Hii nyumba namba 260 ni mali yake na kwa mujibu wa kumbukumbu zetu zilizopo Serikali ya Mtaa, zinaonyesha kuwa mume wa huyo mama alikuwa na biashara na S.H Amon, lakini baadaye walifikishana mahakamani lakini hawa wenye hii nyumba walishinda kesi.

“Cha kushangaza inakuwaje kesi imefika hadi Mahakama Kuu na imeshaamuliwa halafu inakuja tena kwa mlango wa nyuma, mkazi wetu ananyanyaswa, hii si haki, hata nilipowahoji kama wana kibali cha mahakama pia hawakuwa nacho.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: