Napenda kuchukua nafasi hii kutoa ufafanuzi kwa wasanii wote wa Tanzania ambao wamechanguliwa kwenye tuzo mbali mbali zinazoendelea. Hakutakuwa na msaada kwenye tuta wala msaada wowote utakaotolewa ili uweze kupigiwa debe/promosheni maana nimepokea barua pepe nyingi za wasanii wakiomba msaada kwenye tuta ili waweze kutangaziwa namba zao na wapigiwe kura. Promosheni yeyote itakayofanywa katika blog hii italipiwa, ni wewe kuchagua ufanyiwe promosheni ya wiki au mwezi.

Huu ni wakati wa kutambua juhudi za watu na si kuwanyonya hata wale wanaowasaidia ili muweze kupanda. Lipia malipo yako ili uweze kupata huduma zetu kiroho safi. Narudia kusema, hakuna msaada kwenye tuta wala bamsi... lipia nauli yako ili uweze kushushwa kituoni ukiwa salama.

Asanteni kwa kunielewa,

Imetolewa na Uongozi wa Kajunason Media.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: