Hii ni mojawapo ya dalili za mtindio wa mahaba, Unadate na mke wa mtu halafu kwenye Simu umemsevu 'My Husband My All', sasa wewe kimada zogombe ukimuita hivyo unataka mkewe amuiteje labda?? Halafu unampigia simu usiku umemmiss, una akili wewe?? Asipokuona wiki unalalamika heri anakutesa, hebu hurumia watoto wake, anakutesa wewe kama nani?? Kupewa lifti kidogo tu umekuwa bingwa wa kupiga na honi, ukitaka kuteswa vizuri tafuta wa kwako. 

Hivi Wanaume wote hawa mjini sio watamu hadi huyo mme wa mtu ndo ana sukari guru ama?? Halafu umejichanua utadhani we ndo mmiliki vile, sometimes hutaki hata arudi kwa mkewe nguo zote unaloweka, mwenzio kalipiwa mahari wewe utaishia kulipiwa tu kodi, Waza Upya!... My husband My All My Foot... Wezi wa wake za watu halafu mnajiita Independent Women, your just Independent Husband Snatchers!

Na nyie Waume za watu mlioa ili iweje kama bado Mnara hautulii kwenye Wimbi moja???Kama hujamaliza mihamu yako usioe,unatia aibu pete ya ndoa inang'aa halafu unakesha kwa Kimada!

Status hii imetoka Chama Cha Wanaoibiwa Waume Tanzania, Chawawata!

Imetolewa na Mkuu wa Chuo cha Mapenzi
Seth Giovanni
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: