Kamanda wa Polisi mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Charles Kenyela alisema kuwa Taarifa zilizoenea kwamba Bomu limelipuka katika Kanisa la Kilutheri la Kiinjili Tanzania (KKKT), Kunduchi jijini Dar es Salaam zimeenea ndivyo sivyo na kwamba askari walikuwa wanapambana na majambazi.
Wakati taarifa zikiwa zimesambaa katika mitandao ya kijamii na mitaani kwamba kuna kanisa la KKKT limeshambuliwa na bomu hivi punde, Kenyela alisema kwamba taarifa hizo sio za kweli na kwamba askari wa jeshi la polisi walikuwa wanapambana na majambazi karibu na eneo la kanisa hilo. 
Katika mapambano hayo polisi waliwarushia majambazi hayo bomu ili kuyakamata.
"Wakati askari wetu wanapambana na majambazi hayo- waumini wa kanisa hilo wamejitokeza kuwasaidia askari wetu. Naomba unisaidie kukanusha siyo kweli, nitazungumza na vyombo vingine vya habari kuweka sawa," amesema Kamanda Kenyela hivi Punde. 

"Wakati askari wetu wanapambana na majambazi hayo- waumini wa kanisa hilo wamejitokeza kuwasaidia askari wetu. Naomba unisaidie kukanusha siyo kweli, nitazungumza na vyombo vingine vya habari kuweka sawa," amesema Kamanda Kova hivi Punde. 
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: