Balozi wa Palestina nchini Peru na Ecuador, Bwana Walid Abdul Rahim, amesema kuwa nchi mbili hizi zitapiga kura kuunga mkono uanachama wa Palestina kwenye Umoja wa Mataifa mwezi Septemba, mwaka huu.
Rahim aliongeza kusema kuwa hadi sasa Peru inaitambua Palestina kama taifa huru toka mwaka 1947; nayo Ecuador inaitambua Palestina kwa mujibu wa mipaka ya mwaka 1967.
Akizungumza kwenye kikao cha pili cha mabalozi wa Palestina kinachofanyika huko Istanbul, nchini Uturuki Bwana Rahim alisema mkutano huo unafanyika ili kuweka mikakati ya pamoja juu ya suala la Palestina kujiunga na Umoja wa Mataifa mwezi Septemba mwaka huu.
Pia na kufanya jitihada za makusudi kuzishawishi nchi ambazo hazijaitambua Palestina hadi sasa kufanya hivyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments: