Mashindano ya ulimbwende ngazi ya kitongoji kanda ya kaskazini, Vodacom Miss Arusha City Center 2011 yanatarajiwa kurindima Mei 13 katika ukumbi wa Triple A, Arusha.
Akizungumza na blog hili, mratibu wa shindano hilo Bi. Sophia Urio alisema kuwa kwa sasa wamejiandaa vyema tayari kwa ajili ya kufanya uzinduzi huo na mashindano hayo.
Mpaka sasa wamehakamilisha wameshakamilisha mchakato wa kuwasaka warembo wenye mvuto na watahakikisha Miss Tanzania wa mwaka huu wanatokea mkoani Arusha.
Mashindano hayo ambayo yanatarajia kuwakutanisha warembo 10 hakika yatakuwa ya kupendeza sana maana mwaka huu kuna mabadiriko makubwa na mafanikio mengi.
Wadhamini katika shindano hilo ni Vodacom, Startimes, Stone, Shuphaa Quality boutique, Janeths Beaty Parlour pamoja na Africasana Pub iliyopo Holili, Moshi.
Toa Maoni Yako:
0 comments: