CAIRO – RAISI Mahmoud Abbas na kiongozi wa Hamas Khaled Misha’al, jana Jumatano walisaini mkataba wa makubaliano ya kuunda serikali ya umoja wa kitaifa na kumaliza mgawanyiko uliodumu kwa muda mrefu baina ya vikundi vya Palestina.
Akizungumza kwenye hafla hiyo, Bwana Abbas alisema: “Baada ya miaka minne ya giza, akimaanisha mgawanyiko ambao umeleta madhara makubwa kwa maslahi ya taifa, leo hii tumekutana kutimiza ndoto ya wananchi wa Palestina ya kuwa taifa moja ambalo halijagawanyika kwa namna yeyote ile; tukiwa taifa moja lenye nguvu, watu wamoja na jumuia zilizoungana pamoja.”
Wapalestina huko Ramallah washerehekea kusainiwa kwa makubaliano
RAMALLAH --WAPALESTINA jana huko Ramallah walifurahia kusainiwa kwa makubaliano mjini Cairo.
Walipeana vyakula vitamu huku wakipeperusha bendera ya taifa la Misri na kuimba nyimbo mbalimbali kama ishara ya kufurahia jambo hilo.
Mmoja wa wale waliokuwa wakisherehekea tukio hilo adhimu aliliambia Shirika la Habari la WAFA kwamba makubaliano hayo lazima yawe ya kweli na kutosikiliza vitisho vya Israeli.
Mama mmoja wa wafungwa wawili wa Kipalestina alisema alikuja kusherehekea tukio hilo muhimu kwa matarajio kuwa wafungwa wataachiliwa kutoka magereza ya Israeli kwa kubadilishana mateka kati ya Israeli na Hamas.

Toa Maoni Yako:
0 comments: