Wiki hii namleta kwenu chalii anayekuja kwa kasi kwenye muziki wa kizazi kipya. Jina lake anaitwa Abdulaziz Chende lakini kisanii anafahamika kwa jina la Dogo Janja.
Alizaliwa Arusha 1997 katika Hospitali ya Mount Meru. Alisoma Shule ya Msingi Unga Limited na kuhitimu mwaka 2010. Kwa sasa anasoma kidato cha kwanza katika Shule ya Sekondari Makongo. Mengi zaidi kuhusu chalii huyu, ungana nami katika maswali kumi ambayo nilimuuliza.
TQ: Je, hapa Dar unaishi na nani na ni nani anayekulipia ada ya shule?
DOGO JANJA: Naishi na Madee na Tip Top Connection ndiyo wanaonilipia ada.
TQ: Ilikuwaje ukaingia katika familia ya Tip Top na wakaamua kugharamia elimu yako?
DOGO JANJA: Kwanza ifahamike kwamba, Madee siyo ndugu yangu ila alinikuta kwenye shoo Arusha akavutiwa na kipaji changu ndipo walipoamua kunichukua.
TQ: Umri wako bado ni mdogo, imekuwaje ukaingia kwenye fani hii mapema hivi?
DOGO JANJA: Nakumbuka nikiwa darasa la tatu mwalimu wa Somo la Stadi za Kazi alituambia kila mwanafunzi atunge wimbo na aimbe, mimi nilitunga wimbo unaohusu Ukimwi na nikaimba vizuri. Kuanzia hapo nikaanza kuimba muziki huku mwalimu huyo akiwa ananisaidia kwani na yeye alivutiwa na mimi.
TQ: Wazazi wako waliupokea vipi uamuzi wako wa kuingia kwenye muziki hasa ukichukulia kwamba wengi wanadhani muziki ni uhuni?
DOGO JANJA:Walikubaliana nami lakini wakaniambia ‘chonde chonde’ nisiache shule.
TQ: Je, wimbo wako wa kwanza kusikika uliitwaje?
DOGO JANJA: Ulikwenda kwa jina la ‘Sijafikia’ ambao kwa bahati mbaya ulisikika Arusha tu lakini mpaka sasa nina albamu moja inayokwenda kwa jina la Ngarenaro.
TQ: Mpaka sasa kuna mafanikio yoyote ambayo umeyapata kutokana na muziki?
DOGO JANJA: Yapo madogo madogo lakini kikubwa ni kwamba nimepata fursa ya kupata elimu bure.
TQ:Vipi kuhusiana na mchezo wa baba na mama, bado unaundeleza?
DOGO JANJA: Michezo hiyo nimeiacha kitambo, sasa niko ‘siriasi’ na masomo na muziki.
TQ: Hudhani kwamba muziki unaweza kukufanya ukashindwa kufanya vizuri darasani?
DODO JANJA: Kwa hilo sidhani, ninachoamini ni kwamba naweza kufanya vitu vyote kwa wakati mmoja.
TQ: Ni matatizo gani ambayo umekuwa ukikumbana nayo kila siku?
DOGO JANJA: Ni ya kawaida tu, napambana nayo kuhakikisha hayaniharibii malengo yangu.
TQ: Nini matarajio yako ya baadaye?
DOGO JANJA: Ndoto zangu ni kuja kuwa mwanamuziki mkubwa wa kimataifa, naamini hilo litatimia tu.

Toa Maoni Yako:
0 comments: